Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gabo kufungua mwaka 2018 na tamthilia ya ‘Kapuni’

779 Gabo 1 TZW

Fri, 29 Dec 2017 Chanzo: bongo5.com

Msanii wa filamu, Salim Ahmed ‘Gabo Zigamba’ amejipanga kwa ajili ya mwakani kuja kivingine anasema amekuwa akipata maombi mengi na maoni kutoka kwa wapenzi wa kazi zake kuwa mbona haonekani katika filamu mpya lakini kwake ilikuwa ni vema kujipanga na kuja na kitu tofauti ili mashabiki zake wafurahie kazi zake.

Muigizaji huyo ambaye anadaiwa kufanya vizuri kwa sasa, ameiambia FilamuCentral alikaa kimya kwaajili ya kuja na kitu kipya ambacho kitawafanya mashabiki wake kupata burudani mpya.

“Kama kawaida yangu napenda kuwa na maneno machache lakini vitendo vingi tena katika ubora mkubwa sasa mwaka ndio unamalizika ni bora tuupishe na tuamke nao January mwaka 2018 tukirudi vitu bora,”alisema Gabo.

Gabo anasema kuwa kuanzia mwakani atakuwapatia kazi zenye kuelimisha huku pia akisema kuwa amejiongeze kwa kufanya tamthilia ijulikanayo kwa jina la Kapuni na anabadili jina kidogo na kuitwa kwa kizungu kama Mr. Brown tamthilia hiyo itaanza kuonyeshwa katika televisheni mwezi wa kwanza Maishabongo magic.

Chanzo: bongo5.com