Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

G-Nako na mkewe wapata mtoto wa kiume

Gnako Dfs G-Nako na mkewe wapata mtoto wa kiume

Thu, 2 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamuziki G-Nako Warawara jana hii amefunguka kuwa tarehe 22/2/2024 yeye na mkewe Yasinta walifanikiwa kupata mtoto wa kiume.

Hapo awali wawili hawa walikuwa wana mtoto mmoja wa kike "Gianna" hivyo kwa sasa wana watoto wawili.

Story kubwa mitandaoni kwa siku ya leo ni hii na watu wengi wanajadili kwamba G-Nako aliwezaje kuficha siri hii kwa muda wa miezi miwili? Vipi kwa upande wako, katika Dunia ya sasa iliyotawaliwa na mapinduzi ya teknolojia unaweza kuwa na kifua cha kuficha siri ya namna hii?

"Mwenyezi Mungu ni mwingi wa rehema na ni mwaminifu sana, tunamshukuru kwa matendo yake makuu juu yetu tarehe 22/2/2024 saa moja kamili usiku alitujalia kupata mtoto wa kiume na kuongeza familia ya George Sixtus Mdemu," amesema G-Nako Warawara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live