Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Furahi ya Dulla Makabila inaongoza Top Music Videos YouTube

Dullamakabila 1695111967311.jpeg Furahi ya Dulla Makabila inaongoza Top Music Videos YouTube

Fri, 19 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Dulla Makabila ndiye msanii anayemiliki nafasi ya kwanza kwenye chati ya Top Music Videos Tanzania’ ya ‘YouTube Music’.

Wimbo huo ambao audio yake iliachiwa Januari 19, na kutrend hadi nafasi ya kwanza huku ikikusanya zaidi ya watazamaji 900k youtube, video yake iliachiwa Aprili 10. Ndani ya siku 6 video hiyo imetrend miongoni mwa video za muziki zinazoangaliwa zaidi Tanzania.

Baada ya Trend ya siku 6, video hiyo imefanikiwa kuingia kwenye nafasi ya kwanza ya video za muziki 100 zinazotazamwa zaidi YouTube Tanzania.

Ndani ya siku 6 za kwanza, video hiyo imekusanya zaidi ya watazamaji 270,000, huku ikimuweka Dulla Makabila kwenye nafasi ya waimbaji wa singeli wanaoheshimika zaidi YouTube Tanzania.

Video ya Furahi ni filamu fupi ya dakika 3:14, ambayo ndani yake kuna simulizi ya tukio halisi liliotokea mwezi Januari la ndoa ya aliyekuwa mkewe, Zaylisa kuolewa na Haji Manara.

Dulla Makabila aliamua kuachia wimbo huo na video hii nimuendelezo wa pale ilipoishia trend ya audio. Sasa video hii imerudisha ukubwa wa wimbo huo mtaani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live