Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fully story Dudubaya alivyopotea miaka 2, kuzushiwa kifo

Dudubaya Fully story Dudubaya alivyopotea miaka 2, kuzushiwa kifo

Sat, 23 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nakupenda Mpenzi ni miongoni mwa ngoma ambazo zilimtambulisha Dudubaya na kumweka kwenye ramani ya muziki wa Bongo Fleva. Haukosei ukimuita mkongwe, ni legendari kweli kweli.

Dudubaya mika kadhaa iliyopita, alipotea. Story zikawa nyingi, haikujulikana alipokuwa na hadi kufikia hatua baadhi ya watu kuzusha amefariki dunia.

Kupitia mahojiano aliyofanya na Bongo Five, Dudubaya amesimulia kwa kirefu masaibu aliyokutana nayo hadi kujikuta amepotea kwa zaidi ya miaka miwili kutoka mwaka 2020 hadi mwaka jana mwishoni.

“Nilikuwa zangu Mikocheni ndipo nikachomwa na rafiki yangu nikajikuta nimepelekwa kituo cha polisi cha Oysterbay. Nilipofika nikauliza kosa langu ni nini nikaambiwa nimemtukana Joseph Kusaga,” anasema Dudubaya.

Dudubaya anasema, alipofika walimpokonya simu yake na hakuweza hata kuwajulisha ndugu wala jamaa hivyo kujikuta amefikiswa mahakamani ndipo akapewa dhamana lakini hata hivyo alishindwa kupata dhamana hiyo na kujikuta akirudishwa tena sero Oysterbay.

Anasema akiwa polisi, alipangiwa kuripoti Jumatatu, Jumatano na Ijumaa hivyo kumfanya ashindwe hata kufanya shoo za kampeni za aliyekuwa akiwania urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM), hayati John Magufuli.

Kilichofuata hapo ikawa ni kesi kuunguruma mahakamani ambapo Dudubaya anasema alisimama mahakamani kujitetea lakini mwisho wa siku alishinda kutokana na ushahidi kutomtia hatiani.

“Niliwashinda maana hata fomu waliyoiandisha pale ilitaja simu tofauti, mimi simu yangu ni Infinix S4, fomu yao ilisema Infinix 626. Niliuliza nilikutukana nikiwa na nguo gani akasema hakumbuki.

“Nilimuuliza nilikuwa na nywele ndefu au fupi akasema hakumbuki, akaunti yangu ya Instagram wao wakataja Dudubaya wakati yangu ina undaskoo,” anasema Dudubaya. Akizidi kusimulia sakata hilo, Dudubaya anasema, alikuwa anahudhuria mahakamani hadi tarehe 14.9.2021 ndipo hakimu alipoitupilia kesi hiyo kwa kuona haina ushahidi timilifu.

Dudubaya anasema baada ya kushinda kesi hiyo alirudi zake Mwanza na alichagua kukaa kimya kutozungumzia sakata hilo kwenye mitandao wala vyombo vya habari.

“Mimi nimemsamehe Kusaga na nimemuombea pia Mungu amsamehe. Sina tatizo naye, nilikuwa kimya kimuziki kwa sababu nilifungiwa na Basata hivyo nimeshamalizana nao nimerudi upya kwenye gemu,” ndivyo alivyosimulia Dudubaya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live