Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Franco alichapwa fimbo jeshini kumkosoa Rais Mobutu-3

90001 FRANKO+PIC Franco alichapwa fimbo jeshini kumkosoa Rais Mobutu-3

Fri, 27 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Franco Makiadi na bendi yake ya T.P.OK. Jazz, alisaidia sana serikali ya Mobutu katika mambo ya kisiasa kupitia nyimbo zilizokuwa na mafunzo na ushawishi mwingi wa kisiasa. Kutokana na sababu mbalimbali, serikali ya Mobutu ilikuwa makini sana na wanamuziki wake. Kulikuwa watu maalumu wakifanya kazi za kuchunguza kila wimbo ili kubaini ujumbe uliomo kama unakidhi. Mbali na urafiki aliokuwanao kwa rais huyo, ilifikia wakati fulani serikali ikazipiga marufuku baadhi ya nyimbo zake zilizokuwa na ujumbe uliokiuka maadili ya umma. Sifa kubwa ya Franco ni kwamba nyimbo zake takriban zote zilikuwa ni zenye mafunzo kwa jamii, aidha hakusita kukemea hata serikali yake ilipofanya sivyo ndivyo. Franco kuna kipindi alishutumiwa kuimba nyimbo zilizoigusa serikali ya Mobutu ambapo ilimfungulia mashitaka akawekwa jela. Baadaye Luambo akiwa na kundi lake wakavuka mto Kongo unaotenganisha nchi hizo mbili za Kongo - Brazzaville na Zaire, akaenda kujihifadhi kwa muda katika jiji la Brazzaville. Akiwa jijini humo, Rais Mobutu alituma wajumbe kwa ajili ya kumshawishi arudi Kinshasa, akiahidiwa kuwa maisha yake yasingelikuwa hatarini. Bila kufahamu yatakayompata, Franco aliupokea wito huo japo alikuwa ni mwenye kusita, mwishowe akaamua kurudi kama alivyoombwa na kiongozi wake wa nchi. Pasipo kutarajia Franco alipokanyaga ardhi ya Kinshasa, akajikuta yuko matatani tena, akikaribishwa na kikosi cha wanajeshi. Wakamuamuru yeye na kundi lake kupanda kwenye gari lao, wakapelekwa jela ya Ndolo. Huko walikaa kwa muda wa siku mbili, yasemekana walikuwa wakicharazwa bakora za kutosha. Baada ya kutolewa kwenye jela ya hiyo, Franco na kundi lake, wakahamishiwa kwenye kambi ya jeshi ya Tshatshi, ambako walishikiliwa kwa siku kadhaa. Ndipo ikatokea siku rais Mobutu akaenda mwenyewe kujadiliana na Franco Luambo Makiadi. Alimtamkia maneno haya: “Kuanzia leo hii hadi itakapofikia wakati wa mimi kuondoka madarakani, utakuwa ukiniimbia mimi, unatakiwa kunifanyia kazi zangu zote, tena kwa wakati wowote nitakapokuhitaji…” Kuanzia siku hiyo Franco akawa kiungo kikuu hususan katika kampeni zote za rais huyo. Msomaji kumbuka Franco alitunga wimbo wa Candidate Mobutu, ulikuwa ukimsifia rais Mobutu. Kwa ushirikiano huo, Luambo alinufaika sana kuwazidi wanamuziki wengine wote wa nchi hiyo katika kipindi hicho cha utawala wa serikali ya Mobutu Sese Seko Kuku Ngbendu Wa Za Banga. Katika kipindi cha utawala wa rais Mobutu, Franco Luambo Makiadi alitokea kuwa tajiri sana. Purukushani za kisiasa katika nchi yake ya Zaire wakati huo zilipokuwa zikiendelea, Franco alilazimika kuhamia nchini Ubelgiji, akaishi huko na kurekodi nyimbo zake. Baada ya nchi kutulia ikiwa chini ya uongozi wa rais Laurent Kabila, Franco alirudi nchini mwake. Akafanya tamasha kambambe la Festival OK Jazz African Arts lililofanyika Kinshasa mwaka 1966. Rais Mobutu alitawala nchi hiyo tangu Novemba 25, 1966 hadi Mei 16, 1997, akapinduliwa. Kabla yake alitanguliwa na rais wa kwanza wa nchi hiyo, Joseph Kasavubu, aliyekuwa rais tangu Julai 01, 1960 hadi Novemba 24, 1965. Wakati huo Waziri Mkuu wa nchi hiyo alikuwa Patrice Lumumba, aliyekuwa na ushawishi mkubwa kwa Wazaire. Lakini kwa hila, aliuawa katika mazingira ya kutatanisha. Baadaye Kasavubu akapinduliwa na Mobutu, ambaye baada ya mapinduzi hayo, alibadili majina yote yaliyokuwa ya kikoloni likiwamo la nchi iliyokuwa ikiitwa Jamhuri ya Kongo, ikaitwa Zaire. Mji Mkuu uliokuwa Leopodville, ukaitwa Kinshasa. Franco Luambo Makiadi Oktoba mwaka 1971, ndiye alikuwa wa kwanza kutangaza kuwa jina la Jamhuri ya Kongo litabadilika na kuwa Zaire, kupitia wimbo wake wa “Republique Du Zaire”. Kuonyesha mfano kwa wananchi wake, yeye mwenyewe Joseph Sese Seko Kuku Ngbendu Wa Za Banga. Rais huyo baada ya kuingoza nchi hiyo kwa kipindi kirefu, naye alipinduliwa na Laurent Dessire Kabila. Rais Kabila aliongoza nchi hiyo tangu Mei 17, 1997 hadi Januari 16, 2001 alipouawa. Mwanawe Joseph Kabila alichukua nchi hadi alipomaliza kipindi chake, ambapo Felix Tshisekedi akashika kiti cha urais hadi sasa. Mwaka 1978, Luambo akawekwa tena jela kutokana na utunzi wa nyimbo za Helein na Jackie. Nyimbo hizo zilikuwa na maneno machafu yasiyo na maadili kwa umma. Sheria ikachukuliwa kuzipiga marufuku zisipitishwe kwenye radio na TV ya taifa. Franco mwenyewe alijitetea akisema kuwa nyimbo hizo zilikuwa bado hazijaingia sokoni, bali zilikuwa zikiandaliwa kwenye CD. Japo watu walikuwa wakizisikiliza wakati wa maonesho yao kwenye ukumbi wake wa 1.2.3 Kinshasa. Aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa serikali kipindi hicho Leon Kengo wa Dondo, alisimamia suala hilo, na akaamuru Luambo Luanzo Makiadi awekwe jela. Alipelekwa kwenye jela ya Luzubu, iliyopo mkoa wa Bas Kongo, ambao ndiko alikozaliwa Franco. Akiwa jela, Makiadi akawa ni mwenye masikitiko, akijiuliza kisa cha ‘mshikaji’ wake Rais Mobutu kushindwa kumsaidia. Msongo huo wa mawazo ulisababisha kuathirika na ugonjwa wa bawasili, uliomsumbua sana. Miaka michache baadaye, palitokea na mabadiliko kwenye baraza la Mawaziri, ambapo mwanasheria mkuu wa serikali Leon Kengo wa Dondo, alienguliwa wadhifa huo, na akapelekwa kuwa balozi nchini Ubelgiji. Franco baada ya kusikia hivyo, furaha ilimjaa na bila kukawia kamtungia wimbo “Tailleur” wenye tafsiri ya “utabiri wangu watokea kuwa kweli, mdomo wangu kama mganga wa jadi” Luambo baadaye mwaka 1985, alifyatua kibao kikali kilichotikisa nchi cha “Mario”. Kinaelezea mapenzi baina ya kijana msomi lakini hohehahe-mvivu na mwanamama mtu mzima mwenye uhakika wa maisha. Hatimaye kijana alifukuzwa na mwanamama huyo baada ya kumbaini kuwa ni mnyonyaji (mchunaji) asiye na faida yeyote kwake. Kibao hicho cha Mario, kilitia fora ya mauzo na bado kinazidi kuuzika hadi hii leo. Wakati wa maisha yake aliwahi kuongeza uzito ghafla na kufikia paundi 300 ambazo ni sawa na kilo 136. Lakini mwaka 1987 fununu zikaanza kuzagaa kwamba Franco yu mgonjwa. Wimbo aliutengeneza mwaka huo kabla ya kifo chake ulikuwa wa ‘Attention na SIDA ’(jihadhari kwa Ukimwi/ AIDS). Septemba 22, 1989 Franco Luambo Luanzo Makiadi alifanya onyesho lake la mwisho maishani mwake katika ukumbi wa De Melkweg jijini Amsterdam, Uholanzi. Alipoingia ukumbini watu wote waliona kuwa Franco alikuwa katika hali mbaya kiafya. Ilikuwa wazi siku hiyo wapenzi wa Franco walianza kukata tamaa kuhusu afya yake. Siku hiyo onyesho lilianza na kuendelea kwa takribani saa mbili kabla Franco kuweza kupanda jukwaani. Kama ilivyokuwa kawaida MC alikuwa mpiga saxaphone wa T.P.OK Jazz, Isaac Musekiwa, ambaye alikuwa na Franco tangu 1957. Alimsaidia Franco kupanda jukwaani na akamketisha kwenye kiti. Tofauti na umbo lake ambalo lilikuwa kubwa lilokuwa likionekana kama jitu la miraba minne, wakati huo Franco alikuwa amepungua sana, hata kusimama ilikuwa ni matatizo. Wimbo ambao ulikuwa uchezwe ulikuwa ni Chacun Pour Soi, uliokuwa umetungwa na Josky Kiambukuta ambaye siku hiyo hakuwapo. Franco Makiadi alipoanza kupiga gitaa, ikajulikana wazi kuwa ni mgonjwa kiasi cha kushindwa kupiga gitaa hilo. Franco alijitahidi kuimba sehemu zake na kujaribu kusimama, kilipofika kipande chake cha kucharaza gitaa, hali yake ikawa mbaya zaidi, wanamuziki wake walijaribu kumsaidia kusimama. Nguli huyo hakuweza kuendelea kupiga tena muziki kwani alikuwa anakosea kosea hakuwa tena Franco yule waliokuwa wakimfahamu. Ikamlazimu kumshusha jukwaani, akiwaacha wanamuziki na wapenzi wake wakiwa wamechanganyikiwa kwa majonzi. Baadhi yao walikuwa wakitokwa na machozi ukumbini humo. Siku 20 baada ya onyesho hilo tarehe 12 Oktoba 1989 Franco L’Okanga La Ndjo Pene Luambo Makiadi akiwa na umri wa miaka 51, alifariki dunia katika hospitali mjini Namur, nchini Ubelgiji. Mwaka huu imetimia miaka 27, tangu aiage dunia. Mungu aipumzishe roho yake pahala pema peponi, Amina, Mwisho.

Chanzo: mwananchi.co.tz