Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Foby adai kutishiwa kisa kumpenda Zuchu

Foby Zuchu Foby adai kutishiwa kisa kumpenda Zuchu

Fri, 12 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ikiwa ni miezi kadhaa imepita tangu mei mwaka huu, baada ya msanii wa Bongo Fleva na mtunzi wa muziki Foby ameamua kuanika wazi alivyompenda msanii kutoka Lebo ya WCB, Zuchu.

Kupitia kipindi cha XXL kinachoruka kupitia Clouds FM, jana Agosti 11, 2022, Foby alidai kuwa alikuwa amedhamiria na jambo hilo lakini ilifika wakati akaamua kuachana nalo.

Akizungumzia sababu za kuachana na mitikasi ya kumfukuzia Zuchu, Foby amesema ilifika wakati akawa anatishiwa na watu flani kuwa aache hicho anachokifanya.

Foby ameongeza kuwa, baada ya vitisho hivyo kuzidi ilibidi apotezee na kuachana na mpango huo akidai kuwa hana uwezo wa kubishana na wenye nguvu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live