Mwimbaji na mtunzi wa muziki wa Bongo Fleva, Foby amefunguka kuhusu kile alichokiandika kupitia Insta Story yake kumuhusu msanii mwenzake Hamisa Mobetto.
Foby amesema kuwa kitendo alichokifanya cha kuhitaji yeye na Mobetto wamalize tofauti zao haiukuwa ni kuomba msamaha badala yake ni kuwa ameomba yaishe ili kuwepo na amani kati yao na pia sababu nyingine ni kuwa ame-mmiss msanii huyo.
Itakumbukwa, Foby alitumia Insta Story yake kumuangukia Mobetto na kuomba yaishe kwa kile alichoeleza kuwa ame-miss kuona picha zake baada ya kulambishwa block na mrembo huyo kwa takribani miaka mitatu hii ni baada ya kutofautiana.