Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fireboy DML aiponda Afrobeats

Fireboy DML 1 Fireboy DML.

Thu, 29 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Staa mwimbaji wa Nigeria, Adedamola Adefolahan maarufu kama Fireboy DML, ameukosoa muziki wa Afrobeats nchini humo akisema kuwa ni muziki usiojali maudhui (uandishi) na badala yake unabebwa na ‘vibes’ zaidi.

Akiwakosoa wasanii wengine wanaofanya muziki wa Afrobeats, katika mahojiano ya hivi karibuni na Billboard News, mkali huyo wa ‘Vibration’ ameongeza kwamba kwa kiasi kikubwa Afrobeats imeshindwa kugusa maisha halisi ya watu kwasababu umekuwa ni muziki wa kuchezeka (klabu) zaidi kuliko kuibua hisia za ndani za watu wanaosikiliza muziki huo.

‘Tangu mwanzo Afrobeats ilijengewa misingi ya vibes, hata mimi niligundua kuna kitu kimekosekana, hakuna uandishi, hakuna ushairi, ni vibes tu, inachosha sana’ - Fireboy DML

Chanzo: www.tanzaniaweb.live