Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fireboy DML: Nimewahi kufaidi penzi la Madonna

Madonna Fireboy DML Fireboy DML

Thu, 29 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa muziki wa Afrobeats kutoka Nigeria, Fireboy DML amewashangaza mashabiki baada ya kufichua kuwa kipindi anaingia kwenye muziki amewahi kuwa penzini kwa siri na mwanamuziki mkongwe wa Pop wa Marekani, Madonna (65) jambo ambalo hawezi kulisahau katika maisha yake na hakuwahi kulitarajia.

Fireboy (28) amefanya mahojiano na Billboard na kuweka wazi kuwa ni Madonna mwenyewe ndiye aliyemtafuta kwa mara ya kwanza na kumchana kuwa yeye ni shabiki wa muziki wake.

"Alinitumia DM kwenye Instagram na kuniambia kuwa alikuwa shabiki, na kwamba alipenda sana wimbo ambao sikuweza kuujumuisha kwenye albamu yangu ya kwanza," alisema Fireboy.

Mnamo Februari 2022, mitandao mbalimbali ilichapisha picha za Fireboy akiwa na Madonna, wote wawili wamevalia mavazi ya rangi nyeusi. Mwezi uliofuatia, walishirikiana katika Remix ya wimbo wa zamani wa Madonna, unaitwa Frozen.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live