Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Filamu ya Nollywood yasifiwa kwa kuvunja rekodi ya mapato Nigeria

Filamu Ya Nollywood Yasifiwa Kwa Kuvunja Rekodi Ya Mapato Nigeria Filamu ya Nollywood yasifiwa kwa kuvunja rekodi ya mapato Nigeria

Fri, 5 Jan 2024 Chanzo: Bbc

Filamu ya Nollywood nchini Nigeria imevunja rekodi katika chati za filamu, na kuwa filamu ya kwanza ya Nigeria kupata naira 1bn ($1.1m; £900,000) katika kumbi za sinema za ndani.

A tribe called Judah lilipata mafanikio ya kihistoria katika muda wa wiki tatu tu.

Muundaji wake ambaye pia ni muigizaji, muelekezaji na mtayarishaji wa filamu wa Nigeria Funke Akindele - amewashukuru mashabiki wake kwa hatua hiyo muhimu.

"Asante Bwana! Asante Nigeria! Asante Ghana!" alichapisha kwenye Instagram, akipata maelfu ya pongezi.

Rekodi hiyo inamfanya Akindele, 46, kuwa muongozaji mwenye mapato ya juu zaidi wa Nollywood

A Tribe Called Judah inatazamiwa kuzipiku kimapato filamu maarufu za Hollywood katika kumbi za sinema za Kinigeria ikiwemo filamu maarufu ya Black Panther: Wakanda Forever, ambayo hapo awali ilishikilia rekodi kama filamu iliyoingiza pesa nyingi zaidi nchini humo.

"Mafanikio haya sio tu juu ya namba; ni uthibitisho wa uwezo wa kusimulia hadithi, fahari ya kitamaduni, na roho ya kutokukata tamaa," msambazaji wa filamu hiyo, FilmOne Entertainment, alisema kwenye Instagram.

Ikiipongeza filamu hiyo kama "kito cha kitamaduni", Kampuni hiyo pia ilimsifu Akindele, ikisema kujitolea kwake katika kusimulia hadithi "kumeweka sura muhimu katika ramani nzuri ya filamu Nigeria".

Filamu hiyo - ambayo inaonesha mpango wa kuiba duka la mama asiye na mwenza anayelea watoto watano wanaokabiliana na matatizo ya kifedha – ilitokana na historia ya marehemu mama Akindele.

Chanzo: Bbc