Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Filamu ya Idris Kuhusu Mwl. Nyerere Kutoka 2023

Idris Mwalimu Nyerere.png Idris Sultan, Mwl. Nyerere enzi za uhai wake.

Sun, 19 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa filamu nchini, Idris Sultan amesema kwa sasa anaendelea kuandaa filamu (Biopic) itakayozungumzia maisha ya Mwalimu Julius Nyerere ambaye ni Rais wa kwanza wa Tanzania na anatarajia kuitoa mwaka 2023.

Utakumbuka mwaka huu Idris aliandika rekodi ya kuwa muigizaji wa kwanza toka Tanzania kuonekana katika mtandao mkubwa wa kuonyesha filamu duniani, Netflix.

"Ndio filamu ambayo ipo jikoni, ni kitu ambacho imekuwa ni ndoto yangu kubwa sana kuja kufanya Biopic ya Mwalimu Nyerere. Tuipe kama mwaka mmoja na nusu ndio itatoka, mwaka 2022 nina kitu kingine kuhusu Mwalimu Nyerere, hivyo itatoka kwenye 2023," amesema.

"Sidhani kwenye bara la Afrika na nchini za Kusini wanaweza kuongea wao kupata uhuru bila kumuongelea Mwalimu Nyerere na kuitaja Tanzania lakini hatujaongelewa kwenye hilo suala sana, hivyo nitazungumza kwenye filamu," amesema Idris.

Idris ambaye atacheza kama muhusika mkuu wa filamu hiyo, amesema anajua atapitia changamoto nyingi hadi kuikamlisha lakini anaamini ndio filamu itakayompa tuzo ya Oscar ambayo amekuwa akiiwazia miaka mingi.

"Na kwanini nasema nataka nichukulie Oscar kwenye filamu ya Mwalimu, ni kwa sababu itakuwa changamoto kwangu, kwa sababu itanibidi nifanye mabadiliko makubwa sana ili niendane na uhalisia," amesema Idris.

Tuzo za Oscar ambazo zimekuwa zikitolewa nchini Marekani toka Mei 16, 1929 zinatajwa kama tuzo za juu zaidi upande wa filamu duniani na husimamiwa na AMPAS (Academy of Motion Picture Arts and Sciences).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live