Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Filamu ya Harry na Meghan katika mtandao wa Netflix yazinduliwa

Filamu Ya Harry Na Meghan Katika Mtandao Wa Netflix Yazinduliwa Filamu ya Harry na Meghan katika mtandao wa Netflix yazinduliwa

Thu, 8 Dec 2022 Chanzo: Bbc

Mfululizo wa filamu ya Harry & Meghan katika mtandao wa Netflix unaanza Alhamisi na vipindi vitatu hata baada ya kuzua gumzo kali kwa umma na kusababisha utata.

Filamu hiyo inaahidi kufichua ukweli wa simulizi ya ndani ya jinsi Duke na Duchess wa Sussex walijiuzulu kutoka kwa wadhifa wao wa kifalme.

Kionjo cha filamu hiyo kinarejelea "vita dhidi ya Meghan", huku Mwanamfalme Harry akizungumzia "kuvuja na...kuzua mambo" kama sehemu ya "mchezo mchafu".

Jumba la kifalme la Buckingham bado halijajibu madai ya Sussex.

Kutakuwa na uchunguzi mkali wa mfululizo wa filamu hiyo.

Pia "kufichua" maisha ya Ikulu kumeahidiwa, huku Mwanamfalme Harry akizungumza juu ya "maumivu na mateso ya wanawake wanaoolewa katika taasisi hii", katika kumbukumbu dhahiri ya mkewe, Meghan, na mama yake, Diana, Princess wa Wales.

Kionjo cha filamu inapendekeza kwamba itafichua simulizi ya ya mapenzi ya kati ya Mwanamfalme Harry na Meghan yalivyokua.

Lakini pia itaonyesha mabadiliko ya uhusiano na vyombo vya habari na umma.

Hili litakuwa toleo lao la matukio - na wengine wa Familia ya Kifalme wanaweza kuwa wakitazama ili kuona jinsi madai yanavyoenda, ikiwa kuna ushahidi wowote na kama wanapaswa kujibu rasmi.

Chanzo: Bbc