Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Filamu ya "Barbie" yapigwa marufuku Kuwait, sababu ni hii..!

Barbie Film.png Filamu ya "Barbie" yapigwa marufuku Kuwait, sababu ni hii..!

Fri, 11 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Filamu mpya na maarufu ya Barbie iliyotoka mwezi uliopita imefungiwa nchini Kuwait na inatarajia kufungiwa Lebanon kwa kile kilichotajwa kuwa ni uharibifu wa maadili.

Waziri wa Utamaduni wa Lebanon Mohammad Mortada, ameishutumu filamu hiyo kwa kuhamasisha maadili potofu ya jinsia jambo ambalo ni hatari kwa jamii hivyo ameitaka Wizara ya Mambo ya Ndani kuifungia.

Murtada amesema filamu hiyo "inahamasisha mahusiano ya watu wenye jinsia moja, kubadili jinsia, inasapoti watoto kukataa uongozi wa baba, inashusha na kudhihaki nafasi ya mama, na inahoji kuhusu ulazima wa ndoa na kuwa na familia"

Mkuu wa Bodi ya Filamu nchini Kuwait Lafi al-Subaiei amesema kuwa kwa kawaida wanapoona mambo yanayoenda kinyume na tamaduni zao huwataka waandaaji kuviondoa vipande husika.

Lakini ikiwa filamu zinahamasisha mambo ambayo nchi hiyo haikubaliani nayo huwa wanazifungia kwa haraka.

Tangu izinduliwe rasmi mwezi uliopita, filamu hiyo imekwisha tengeneza zaidi ya dola za Kimarekani Bilioni 1 Duniani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live