Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fiesta yarejea kwa kishindo, kuanza kuunguruma Sumbawanga

WhatsApp Image 2022 09 05 At 08.jpeg Fiesta yarejea kwa kishindo, kuanza kuunguruma Sumbawanga

Mon, 5 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa Msimu wa Fiesta 2022 Sebastian Maganga a.k.a Boss Seba amesema kuwa Mkoa wa Sumbawanga umepata heshim a ya kuzindua msimu wa tamasha la Fiesta litakalofanyika Septemba 17 katika Uwanja wa Nelson Mandela.

Mwenyekiti huyo wa Kamati ya Fiesta amesema hayo jana usiku Septemba 4 kwenye uzinduzi uliofanyika mwenye yadi ya Makontena ya Anko Tajiri iliyopo barabara ya Nyerere Jinini Dar es Salaam.

"Huu ni msimu wa shangwe na burudani hivyo ni wakati wa watanzania kujumuika pamoja na kusherehekea" amesema Maganga.

Kwenye uzinduzi huo wasanii waliopanda jukwaani ambapo yalitengenezwa kwa ubunifu wa kutumia makontena ni pamoja na Wozu, Rayvanny, kundi la wasanii Weusi ambapo Msanii Joh Makini amesema kuwa anawaahidi mashabiki wao kuwaonyesha mambo mapya kwa sababu wao kupata nafasi hiyo haikuwa bahati mbaya kwani wao wamekuwa ni wabunifu na kuwa wakibadilika kama gari aina ya Mercedez Benz.

Wasanii wengine ambao walitambulishwa ni pamoja na Ney Wa Mitego,Country Boy, Abdu Kiba, Dogo Janja,Kayumba, Sarafina, Aika na Navimenzo,Maarifa.

Aidha Maganga amesema kuwa "Tulizindua mwaka mpya wa burudani sambamba na kurudi kwa msimu wa Fiesta ambapo huu ni mwaka wa 18 tulitoa fursa kwa ndugu,marafiki, wadau wa burudani pamoja na wafanyakazi wa Clouds kukusanya maoni yao yalikuwa mengi tukakaa Kamati na kuyachuja"amesema Maganga.

Maganga ameitaja baadhi ya Mikoa mingine ambayo itafuata katika mnyororo wa Msimu wa Fiesta kuwa baada ya Sumbawanga msimu wa fiesta utafanyika Mkkani Tabora baadaye Mwanza, Dodoma,Arusha,Mtwara na Dar es Salaam huku kauli mbiu ya msimu wa fiesta ni weka maneno.

"Kuna uwezekano mkubwa mikoa ikaongezeka huku akisema kuwa wasanii wengine ambao watashiriki kwenye msimu wa Fiesta ni pamoja na Ali Kiba, Mr.Blue, Juma Jux,Kusa ,Jay Melody, Dulla Makabila, Mario' amesema Maganga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live