Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Feza Kessy na mwanaye wazua gumzo

Feza Kessy M Feza Kessy na mwanaye wazua gumzo

Wed, 19 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshiriki wa Big Brother Africa msimu wa nane (2013) na Mwanamuziki Feza Kessy ameshitua watu wengi baada ya ku-post picha akiwa na mtoto wake wa kiume.

Watu wengi wamepata mshangao huo baada ya kufahamu kuwa Feza Kessy ana mtoto mkubwa wakati wao walikuwa wakidhani Mwanamuziki huyo ni mdogo kiumri, hivyo hata kama ana mtoto basi atakuwa mwenye umri mdogo.

Mastaa mbalimbali na watu wengine wamempongeza Feza Kessy kwa kuendelea kumlea vyema mtoto wake mpaka hivi sasa alipofikia.

Kwa mujibu wa Wikipedia, Feza Kessy alizaliwa Agosti 24 1988, hivyo Mwezi wa Nane mwaka huu anatarajia kutimiza miaka 36.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live