Mwezi Mei mwaka 2021 mwimbaji wa Tanzania @fezakessy alitangaza rasmi kusainiwa na label ya nyota wa Muziki nchini Nigeria, D’Banj. Lakini ni Kipindi kirefu kimepita na hakukuwa na kazi yoyote chini ya label hiyo.
akihojiwa juzi kwenye XXL Clouds FM, Feza ameanika wazi kwamba menejimenti yake hiyo ilimpiga 'STOP' kuimba nyimbo za Kiswahili au kuwaimbia Watanzania, zaidi ajikite Kimataifa kwa kuimba Kiingereza na nyimbo zenye mahadhi ya Nigeria.
Mwanadada Feza anasema aliamua kuweka mgomo mpango huo na aliwekwa benchi kwa muda.
Ni kama ametaka kuwaaminisha juu ya nyimbo za Kiswahili, Feza juzi ameachia ngoma yake mpya “SIWEZI” mikono ya Mtayarishaji Gachi B.