Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fella: Wasanii wengi wa Temeke wana mawazo mgando, ni wajuaji

Fellaa2 Mkubwa Fella

Sat, 23 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja Diamond Platnumz na Mkurugenzi wa Yamoto Band, Mkubwa Fella amesema wasanii wengi wanaoiwakilisha Temeke (TMK) wana mawazo mgando hasa linapokuja suala la kutimiza ndoto zao.

Fella amesema amekuwa akijitahidi sana kuwashika mkono wasanii wanaotokea maeneo ya Temeke lakini wengi wao wamekuwa wakijifanya wajuaji kwa kushindwa kufuata ushauri wanaopewa.

Aidha, Fella amesema kuwa ili msanii aweze kusainiwa katika Mkubwa na Wanawe hana utaratibu wa kupokea CD badala yake amekuwa ni mtu ambaye anampa nafasi msanii ya kuimba mbele yake na kumsikiliza akivutiwa naye anamsaini lakini akishindwa kuvutiwa naye anamsaidia kwa namna nyingine.

Mbali na hilo pia mkubwa Fella amegusia ishu ya kuwajengea nyumba wasanii Chege Chigunda, Temba pamoja na Juma Nature akibainisha kuwa ni juhudi zake pamoja na kusimamia misingi ya nidhamu ndiyo iliyomfanya hadi akafanikiwa kuwajengea nyumba zao wasanii hao.

Alipoulizwa kuhusu ishu ya kuhusika kumuondoa Harmonize ndani ya WCB, Mkubwa Fella amesema siyo kweli lakini anatamani siku zote watu wawe wakweli waongee ukweli binafsi yeye anachukia sana uongo na watu waongo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live