Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fella: Hata wakiungana, harmonize na Rayvanny hawamuwezi Diamond

Harmo Rayvanny Sd Fella: Hata wakiungana, harmonize na Rayvanny hawamuwezi Diamond

Tue, 5 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja wa Msanii Diamond Platnumz na CEO wa Band ya Mkubwa na Wanawe, Mkubwa Fella amesema kuwa hata kama Harmonize na Rayvanny wataungana, bado hawawezi kushindana na aliyewahi kuwa bosi wao, Diamond Platnumz.

Fella amesema hayo baada ya Harmonize na Vanny Boy kuvunja bifu lao baada ya kumaliza bifu lao na kupatana.

“Hivi unajua kama ERayvanny ametokea Miubwa na Wanawe? Kwa hiyo huyo Rajab ambaye sasa ni Harmonize katokea kwangu ndipo akaenda WCB, kwa hiyo wote wametokea kwenye koo yangu.

“Lakini hawa Diamond hawamuwezi labda nife mie, lakini kama nipo hai hawamuwezi, au labda nisiwepo maana kuna leo na kesho. Kikazi, kifedha vyote hawamuwezi," amesema Mkubwa Fella.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live