Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Faraja Nyalandu atwaa tuzo ya mwanamke mhamasishaji

50817 Pic+nyalandu

Sun, 7 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Aliyewahi kuwa Miss Tanzania mwaka 2004, Faraja Kota ametwaa tuzo ya malkia wa nguvu katika kipengele cha mwanamke mhamasishaji.

Faraja amepata tuzo hii leo Jumamosi April 6, 2019, katika ukumbi wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam ambapo tuzo 20 zinatarajiwa kutolewa.

Faraja ambaye ni mke wa aliyewahi kuwa waziri wa maliasili na utalii, Lazaro Nyalandu, amepata tuzo hiyo kupitia mradi wake wa Shule Direct .

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo, amesema kwake ni heshima na mzigo.

Ameongeza alichojifunza ni kuwa kila mtu ana kusudi na thamani ambapo akitupia fursa thamani yake inaweza kushangaza dunia.

"Kikubwa ni kuhakikisha tunamtanguliza Mungu mbele na kutembea katika kusudi lake," amesema.

Wengine ambao tayari wamekabidhiwa tuzo ni Elizabeth Swai, Edna Kiogwe na Julieth Joseph katika kipengele cha kuongeza thamani ya mazao.

Tuzo hizo ambazo hii ni mara yake ya tatu kufanyika zimehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na aliyewahi kuwa Rais wa Bunge la Afrika, Gertrude Mongela.



Chanzo: mwananchi.co.tz