Familia ya marehemu Notorious B.I.G imelimaliza shauri dhidi ya familia ya mpiga picha Chi Modu juu ya picha maarufu ambayo ilipigwa miaka ya 90 kwenye Maghorofa ya World Trade Center. Kwa mujibu wa Billboard, Staci Jennifer Trager ambaye anaiwakilisha familia ya marehemu Biggie, ametangaza juu ya kumalizika kwa shauri hilo, Alhamis Januari 18 mwaka huu.
Wakati vipengele vya makubaliano yao vikiwa havijaanikwa wazi, Trager amefafanua kwamba makubaliano hayo yalikuwa kati ya mtoto wa Biggie na mjane wa Modu. Kumbukumbu zinaonesha Modu ambaye alifariki mwaka 2021, alipiga picha hiyo miaka 5 kabla ya Jengo hilo kuanguka Septemba 11, 2001.
Shauri hilo lilifunguliwa mwaka 2019 ambapo familia ya Biggie ilidai kwamba Modu aliisajili picha hizo isivyo halali (illegally) kwa matumizi ya mitandao kama NFTs kinyume cha sheria au matakwa ya mmiliki ambaye ni Christopher Wallace maarufu kama Notorious B.I.G.