Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Familia yafunguka Mr Ibu kukatwa mguu

Mr Ibu Familia yafunguka Mr Ibu kukatwa mguu

Mon, 18 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Familia ya muigizaji mkongwe wa Nigeria, John Okafor almaarufu Mr Ibu imejitokeza kufafanua kuhusu uvumi kwamba msanii huyo amekatwa miguu yake yote.

Familia hiyo imefutilia uvumi huo ikiweka wazi kuwa ni mguu mmoja tu wa muigizaji huyo ambao ulikatwa mwezi uliopita.

"Tunapenda kutoa shukurani zetu za dhati kwa Wanigeria na umma kwa ujumla kwa mchango wenu mkubwa, wa kimwili, kiroho na zaidi ya yote kifedha kwa kumfanya baba yetu John Okafor (Ibu) asimame," familia imesema katika taarifa.

Katika taarifa hiyo iliyoshirikiwa kwenye akaunti rasmi ya Instagram ya muigizaji huyo, familia hiyo ilithibitisha kwamba hata hivyo kulikuwa na kukatwa kwa mara ya pili kwenye mguu huohuo ambao ulikatwa mwezi uliopita.

"Tunataka kurekebisha madai potofu yanayoenea kwenye mitandao ya kijamii kuhusu hali ya sasa ya afya ya baba yetu. Kwanza tungependa kusema kwamba baba yetu hakukatwa miguu yote miwili bali mmoja tu.

Kukatwa kwa mara ya kwanza hakukusahihisha kabisa hali yake ya kiafya kwa hivyo daktari alilazimika kwenda mbele kumkata mguu huohuo ili kuhakikisha hatumpotezi,” iliongeza taarifa hiyo.

Ikifafanua kuhusu ugonjwa wa muigizaji huyo, familia hiyo imesema chanzo cha ugonjwa wa baba yao siyo ugonjwa wa kisukari lakini alikuwa na damu iliyoganda mara kwa mara kwenye mguu wake (mishipa yenye ugonjwa) na changamoto nyingine za kiafya zilizohatarisha maisha yake.

Familia ilibainisha kuwa haijampeleka muigizaji huyo mkongwe nje ya nchi kwa matibabu zaidi kwani daktari amemtangaza kuwa hafai kusafirishwa kwa ndege.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live