Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Familia: Hatujui Muna Anaendeleaje

Muna2.png Familia: Hatujui Muna Anaendeleaje

Tue, 15 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

FAMILIA ya mwanamama Muna Love ambaye anasemekana kuwa hali yake ni mbaya baada ya upasuaji (sajari) kibao za kurekebisha maumbile ya mwili wake kudunda.

Muna Love ni mwigizaji wa Bongo Movies na Mtumishi wa Mungu kama ambavyo amekuwa akijinasibu, lakini amekuwa akilitafuta umbo la ndoto yake kwa kufanya upasuaji (sajari) kila kukicha kwa ajili ya kurekebisha maumbile ya mwili wake.

Hata hivyo, hivi karibuni alishtua wengi baada ya kusema kuwa anajuta kufanya sajari na kutubu kwa Mungu wake akiwaomba Watanzania wasijaribu kufanya hivyo.

Kwa mujibu wa dada yake ambaye aliomba hifadhi ya jina, Muna Love ni mdogo wake, lakini wao kama familia hawajui anaendeleaje kiafya baada ya kutangaza kuwa na hali mbaya.

“Kwa kweli hatujui maana sisi hajatuambia kama anaumwa na hiyo sajari aliyoifanya hakutushirikisha kwa hiyo kuhusu mambo yake sisi kama familia hatujui lolote labda muwaulize rafiki zake.

Katika hali ya kushtua, dada huyo ameibua madai ya muda mrefu kwamba, Muna Love aliikataa familia yake hivyo familia nayo ikawa haimtambui.

“Ni ukichaa wake tu, wala hatukumkosea naona alivyopata pesa akaona labda hatuna hadhi ya kuwa naye kwa hiyo akaamua kutukataa.

“Tunachojua muda utaongea, pesa zikiisha atatukumbuka, kwa sasa haoni umuhimu, lakini sisi ndiyo tutakaomlilia na kumzika,” anamalizia dada huyo.

Kwa upande wa baadhi ya wafuasi wake kwenye mitandao ya kijamii wamekuwa wakimtabiria mambo mabaya ikiwemo kifo kwa maelezo kwamba, mambo hayo anayoyafanya ni namna ya kumkosoa Mwenyezi Mungu na ndiyo yatakuwa mwanzo wa umauti wake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live