Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fally Ipupa kukiwasha Dar kesho

Picha Pg 20 Fally Ipupa kukiwasha Dar kesho

Fri, 8 Oct 2021 Chanzo: ippmedia.com

MSANII wa muziki wa dansi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Fally Ipupa, amesema anajisikia fahari kufanya onyesho lake la kwanza jijini Dar es Salaam, baada ya kuzindua albamu yake mpya.

Fally Ipupa kesho anatarajia kufanya onyesho jijini Dar es Salaam, ambapo ameahidi kutoa burudani ya kiwango cha juu kwa mashabiki wake na mashabiki wa muziki huo wa dansi.

"Ni mara ya kwanza nafanya onyesho baada ya kuzindua albamu yangu ni fahari kwangu kuona Tanzania ndio nchi ya kwanza kutembelea katika mpango wangu wa kuzunguka baadhi ya nchi za Afrika kutangaza alabamu yangu," alisema Ipupa.

Alisema kuwa yeye na wanamuziki wake wamejipanga kutoa burudani ya uhakika kwa mashabiki wake kwa kupiga kuanzia nyimbo zake za nyuma na nyimbo zilizopo, kwenye albamu yake mpya.

Kwa upande wake mratibu wa maonyesho ya mwanamuziki huu yatakayofanyika Dar es Salaam (leo) na jijini Mwanza siku ya Jumatano, kutoka kampuni ya Primetime promotion, Edward Lusala alisema mashabiki wa muziki huo, wajiandae kwa ajili ya burudani ya uhakika kutoka kwa msanii huyo.

"Tunashukuru sana ushirikiano kutoka kwa washirika wetu kampuni ya Startimes, ambao nao wamefanikisha kufanyika kwa onyesho hili kesho (leo) hapa Dar es Salaam na baadae Mwanza," alisema Edward.

Aidha, Mkurugenzi wa masoko wa Startimes, Tangji Yu, alisema wanafarijika kuwa sehemu ya waandaaji wa onyesho la mwanamuziki huyo, ambapo kampuni yake inafanya hivyo kuwapa burudani wateja wake.

Fally Ipupa ambaye amewahi kushirikiana na msanii wa Tanzania, Diamond Platinumz kwenye wimbo uliyopata umaarufu mkubwa ya 'Inama', leo anatarajia kukonga nyoyo za mashabiki wake, kwenye ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam.

Chanzo: ippmedia.com