Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fally Ipupa atoa pole familia za watu 11 waliofariki katika tamasha lake

Fally Fally Ipupa atoa pole familia za watu 11 waliofariki katika tamasha lake

Mon, 31 Oct 2022 Chanzo: BBC

Mwimbaji wa Congo Fally Ipupa amezipa pole familia za watu 11 waliofariki siku ya Jumamosi wakati wa tamasha lake katika uwanja mkubwa zaidi wa michezo katika mji mkuu, Kinshasa.

Uwanja huo ulikuwa umejaa kupita uwezo wake wa watu 80,000 - hata vijia vya eneo hilo zilikuwa zimejaa, kulingana na mtu mmoja aliyeshuhudia tukio hilo.

Ripoti zilisema ukubwa wa umati wa watu ulizidi kwa kiasi kikubwa idadi ambayo maafisa wa usalama wanaweza kudhibiti.

Maafisa wawili wa polisi walikuwa miongoni mwa waliouawa. Waziri wa mambo ya ndani nchini humo Daniel Aselo Okito ametaka waandalizi kuadhibiwa kwa kukosa kuweka ukomo wa idadi ya watakaohudhuria tamasha hilo.

Katika ujumbe wa Facebook, Fally Ipupa alisema kulikuwa na "uzingatiaji madhubuti wa taratibu za usalama" katika tamasha hilo.

Aliongeza: "Nimefadhaika sana na ninatuma rambirambi zangu kwa familia zote. Mungu kwa rehema zake nyingi aifariji mioyo iliyofiwa."

Chanzo: BBC