Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Faiza ampongeza Baba Levo kumthamini mchepuko kuliko mke

Baba Levo Faiza Mama Ruby Faiza ampongeza Baba Levo kumthamini mchepuko kuliko mke

Thu, 18 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwigizaji wa Bongo Movies na mjasiriamali, Faiza Ally amempongeza mtangazji wa Wasafi FM, Revocatus Chipando kama Baba Levo kwa kuamua kumthamini mchepuko wake aitwaye Asmah baada ya mkwe aitwaye Salma Mdoli au Mama Ruby kumfanyia vurugu.

Kauli hiyo ya Faiza inakuja ikiwa ni siku moja baada ya Babab Levo kufunguka kuwa mkewe huyo amemfanyia fujo mchepuko wake Asmah baada ya kumletea zawadi zenye tahamni ya Tsh 400,000 kutoka China huku akimletea mkewe zawadi zenye zaidi ya Tsh milioni 10.

"Kama ungeamua kumsikiliza Baba Levo vizuri kwa kutaka kuelewa ungemuelewa, kama ukimsikiliza kutaka kumjaji hutuelewa kabisa, binafsi nimemuelewa.

"Mimi nimependa anavyosimama kwenye ukweli japo inaonekana anampenda mama Ruby lakini amesimama kiume kweli, yaani huyu ndio mwanaume hasa! Yaani huyu anafaa kuoa hata wake wa 4 na akasimamia vizuri kabisa.

"Wanawake tuna tabia ya kuyumbisha wanaume, huyu anaonekana hayumbishwi! Sijui historia ya nyuma lakini kutokana na maelezo aliyoyatoa, yuko sawa kabisa labda kama sio kweli!

"Wewe mke umeondoka nyumbani mwaka, umeacha watoto nyumbani wa kike, lazima unapoondoka gape lako lizibwe. Angewezaje kulea watoto tena wa kike bila mke nyumbani?

"Asmah hana kosa kacheza nafasi yake vizuri kama mke, kalea watoto katulia baada ya mwaka unataka kurudi mwenzio katolewa kwa ajili yako kwa sababu wewe ni mke na ni mama.

"Na wewe ndio umechaguliwa! Mpaka hapo si sawa kisheria, Asmah tayari ni mke! Lakini umethaminiwa wewe ukarudishwa mwenzio katolewa. Je, ulitaka Baba Levo am-damp?

"Kama kisicho faa wakati amemlelea wanae mwaka Mzima? Yaani mimi ningekua wewe kwa kweli kwanza ningemshukuru mume wangu kwa kunirudisha nyumbani kama mke maana hapo tayari umesha mzidi Asmah ningekutulia tu nicheze nafasi yangu kama mke huku nikiendelea kuomba Mungu mume wangu awe wangu tena.

"Ningemuombea na huyu Asmah apate wake aniachie wangu! Hongera Baba Levo kwa kutokumuacha Asamha kama kitu kisichofaa na kumuhifadhi na kumlinda kama mwanamke anaestahili heshima pia.

"Ndoa itabaki kuwa ndoa lakini kila mwanamke hata asiyeolewa ana stahili kuheshimiwa pia. Pia Hongera hata ulipoachana na Mama Ruby bado ulismamia Familia kama inavyopaswa kuwa.

"Mimi baada ya kusikiliza interview yako nimeoma katika wanaume wa maana na wenye misimamo wewe ni wa maana sana yaani kwa sababu wewe ni Mkristo lakini kama ungekua Muislam ningeshauri uoe wote wawili maana unawamudu.

"Wako wanaume wengi wapuuzi eti kwa sababu tu ameoa mke wake hata afanye madudu vipi, anajifanya kipofu hata kama anaona anakosea bado yuko upande wake!

"Hiyo sio adabu ni ujinga! #temporalypost @mwijaku, Baba Levo yuko sawa yako yakujifunza mengi kwa wanaume na wanawake kupitia Baba Levo," amesema Faiza.

Kwa upande wa Baba Levo yeye amesema;" Suala la kumuacha Asmah siwezi kushauriwa na Mama Ruby, ni mimi mwenyewe niamue."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live