Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Faiza amlipua Diva "Wewe ni feki, nakuzidi kila kitu mpaka akili"

DIVA NA FAIZA Faiza amlipua Diva.

Tue, 29 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya mtangazaji wa Wasafi FM, Diva the bawse kumlipua msanii wa Bongo Movies na mjasiriamali, Faiza Ally amejibu mapigo.

Faiza kupitia ukurasa wake wa Instagram amesema; "Wewe ni feki kuanzia rangi yako ya mwili mpaka picha zako ni feki, umepata na mume feki. Nimerudi hewani nasikia habari juu juu tu. Diva mimi mtu akinianzaga simalizagi kama una kumbukumbu ulianzaga wewe kuniongelea kwenye interview mimi najibu tu.

"Ulianza wewe kuniposti mpaka unaposti na wapinzani wangu ili unitoe tu kwenye reli kumbe ligi lenyewe huliwezi, narudia tena kweli we ni mnafiki! Kweli una mawigi feki na kweli we ni mshamba.

"Kama haya maneno ni kesi nipeleke Mahakamani mimi niko Tanzania, kama wewe una ruhusa ya kuniongelea basi na mimi ninayo! Kama huna na mimi sina, wewe ulianza mimi naendeleza, halafu wewe hunishindi chochote.

"Wewe umeajiriwa ni mfanyakazi wa mtu, mimi nimejiajiri Boss mwenyewe, wewe umepanga mimi nimejenga! Tena sina nyumba moja, Diva nimekushinda vingi mpaka kulipa ada! Nimekushinda mpaka mawigi original.

"Wewe ni feki kuanzia rangi ya mwili, mpaka picha zako feki, nguo miwani zako feki, kwendraaaaa peleka ujinga wako huko pumbavu! Nakukumbusha kabla hujatafuta Mwanasheria kajisikilize upya alafu umwambie Mwanasheria wako wewe ndio ulianza.

"Nilikuwa nimesahau nimekuzidi akili mpaka uzuri, maisha feki mpaka umepata na mume feki! Jinga kabisa wewe na hereni zako kubwa kama mang'ati," amejibu Faiza Ally.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live