Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Faiza achekerea ndoa ya Sugu na Happy kuvurugika

Ndoa Suguuu(1) Faiza achekerea ndoa ya Sugu na Happy kuvurugika

Tue, 17 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tetesi za ndoa ya msanii nguli wa rap na mwanasiasa, Joseph Mbilinyi 'Sugu' na mkewe, Happiness Msonga kutetereka, zimemuibua mzazi mwenzake na Sugu, Faiza Ally ambapo amesema "naomba wakaangwe mpanga wachakae"

Faiza ameandika haya:

"Ushauri wa bure kwa wanawake msitumie nguvu kubwa kutenganisha watu na wapenzi wao! Msitumie nguvu kubwa kuolewa na mtu ambae moyo wake uko kungine, usiroge sana kumpumbaza mtu, akishtuka madhara yake ni makubwa kuliko kuwa single.

"Tumia nguvu kubwa kujiimarisha kuwa bora zaidi ya Jana , bora uroge upate hela sio mapenzi , mapenzi ni kitu halisi hakina mbambamba kabisa Eeh baba watu wana post na kufuta maana picha hazina uhusiano.

"Halafu nyie washauri kuanzia marafiki mashemeji mama wake maboss na mawifi wkt mtu moyo wake una teseka Nyie hamkogo tena mkisha toa ushauri wa hivyo na ku destroy mioyo watu.

"Mambo yakiharibika wala hamuhusiki hebu mue mna acha watu wafate mioyo yao! Eeh Mungu naomba wasiachane yaani wajikaange mpaka waungue, yaani mpaka wakiachana wawe wamechakaa mpaka hawatizamani.

"Kweli malipo duniani hamna cha ukifa wala kufufuka Yaani unalipwa kulingana na matendo Alhamdullilah, tujitahidi kuwa watu wema Jamani tulipwe wema Mungu hakopeshi anakupa muda tu wa kijitafakari na huruma akiona huelewi anakupa una chostahili," amesema Faiza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live