Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Faiza: Sijasoma lakini nimewazidi wengi

Faiza Allyyy Faiza: Sijasoma lakini nimewazidi wengi

Fri, 9 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Faiza Ally; ni staa wa Bongo Movies na mjasiriamali wa Bongo ambaye ametoa mazito akisema kuwa, pamoja na kwamba hajasoma, lakini amewapita wasomi wengi.

Faiza anasema; “Nimezaliwa miaka 38 nyuma kutoka mtaani mpaka nilipo leo, sina jina la baba, mama wala elimu yoyote, sina urithi wa wazazi wala sitegemei wa mume…kwa hiyo maisha yangu hayakuwa rahisi, sura yangu isikudanganye.

“Halafu nimewapita wasomi wengi tu na baba zao na mama zao na waume zao na wake zao kuanzia sura zao mpaka maisha yao, wenye hela na majina...sura yangu au maisha yangu usichukulie poa…nyuma yake kuna mishale mingi sana naendelea kukwepa.

“Machungu mengi na furaha na mfanikio pia … Kama unavyojua maisha yalivyo magumu na bado mbishi, kwa hiyo vitu vya hovyohovyo havinishtuagi….”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live