Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Faiza: Sasha sio sawa na Paula

Paula Sasha Faiza: Sasha sio sawa na Paula

Thu, 25 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa Bongo Movies na mjasiriamali, Faiza Ally amesema kuwa mwanaye Sasha si sawa na Poaula wa Kajala kwani kila mtu amezaliwa na kuishi kwa namna yake kulingana na mipango ya Mungu.

Faiza amesema wanaomsema Paula na mama yake Kajala wanakosea kwani binti huyo na ni mtu mzima ambaye anayo haki ya kuamua jambo lolote hata mahusiano bila kulazimishwa na mtu.

"Hili swali huwa naulizwa mara nyingi sana kwamba je ningependa mwanangu awe kama Paula? Nikicheza na Mwanangu naambiwa namtengeneza Paula, najibu kwa pamoja, Paula na Sasha ni binadamu wawili tofauti, kwa imani yangu kila binadamu ana stori yake iliandikiwa.

"Ukiniuliza kuhusu Paula nitakwambia ni binti wa kawaida kama wengine wote, Paula ni msichana wa zaidi ya miaka 18 ana haki na uhuru wa kuwa na anaemtaka.

"Zamani wazazi wetu waliolewa kuanzia miaka 10 na zaidi, mtaani watoto kama Paula wana watoto na mabwana wa kutosha, Paula amebahatika kuwa Star na siyo tu kuzaliwa na Star kwasababu wazazi wake ni Mastaa hivyo habari yake ya bwana ni habari ya kitaifa.

"Kiufupi Khan (Mtangazaji wa Clouds Media) ni mzalilishaji kwa njia ya maneno, Paula hana ajabu katika anayoyafanya ajabu inakuwa ajabu kwenye macho yenu kwasababu mnaona na picha, lakini huko mtaani mnafanya makubwa zaidi ya Paula.

"Paula mwanangu, kuwa jasiri mama wewe ni Star siyo mtu yoyote, kweli kuna wakati nilichukizwa juu ya mapenzi yangu kwa Fahyma lakini haya yamepita mimi ni mmoja kati ya watu wanao mpenda sana Fahyma, na familia yake na sasa nimefurahi sana wako pamoja Alhamdulillah wadumu.

"Na wewe utapata njia yako, bado ni msichana mdogo mzuri dunia yako binti yangu najua uko kwenye age ya moto sana, utapatwa na mengi mno, tumia akili zaidi utafika mbali, hawa wanaokuona unakosea leo kesho watakupigia makofi, kuna siku, stay strong and focus," amesema Faiza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live