Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fahyma afunguka ndoa yake na Rayvanny

Fahyma Rayvanny Jk.jpeg Fahyma afunguka ndoa yake na Rayvanny

Sun, 23 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Fahyma; Ni mrembo hasa lakini sifa kubwa ambayo inamfanya aendelee kuonekana mrembo kila kukicha ni heshima na upendo wa dhati alionao kwa watu hususan mashabiki wake, mara kadhaa baba wa mtoto wake msanii wa Bongo Fleva, Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’ amekuwa akinukuliwa akimsifia mwanamke wake huyo kuwa ni mrembo kwelikweli na ni mama anayejitambua hivyo hafikirii kuachana naye.

Van anasema haachani naye leo wala kesho licha ya kuwa kuna baadhi ya watu wanatamani penzi lao livunjike hata kesho.

Yes! Si mwingine, hapa namzungumzia Fahyma binti mwenye umri mdogo lakini mkubwa kifikra,

Showbiz: Sasa unajishughulisha na nini? Maana tumezoea tu kukuona mitandaoni ukitupia picha zako.

Fahyma: Unajua mimi nafanya mambo mengi sana ambayo watu wengi hawawezi kuyafanya, lakini huwa sipendi kuyaanika hadharani, hata mume wangu analijua hilo, anafahamu kuwa sipendi mambo yangu kila mtu ayajue lakini ukweli ni kwamba mimi nina plan za kufungua kitu flani kuhusiana na mambo ya mavazi, pamoja na urembo, hivyo Mungu akijaalia hivi karibuni nitakuja na ‘product’ yangu mwenyewe ambayo itakuwa ni brand yanfayvanny.

Showbiz: Kuna kipindi uliandika maneno kwenye akaunti yako kuwa wewe na Rayvanny tayari mmeshafunga ndoa, hivyo ni mume wako halali lakini kitu ambacho mnakisubiri sasa hivi ni sherehe tu, je ni kweli au uliamua tu kufanya hivyo kwa lengo la kuwakomesha wanaofuatilia penzi lenu?

Fahyma: Ni kweli mimi na Rayvanny tayari tulishafunga ndoa, ila bado tu kufanya sherehe, nadhani hicho kitu watu hawakijui ndiyo maana nikaandika vile kwenye akaunti yangu ili watambue na waache kuzungumza mambo wasiyoyafahamu.

Showbiz: Sasa Fay sherehe itakuwa lini?

Fahyma: Sherehe siwezi kuitaja itakuwa lini, lakini ikiwa tayari kila mtu atajua kwa sababu nitaweka wazi haitakuwa siri tena.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live