Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fahyma: Sina mpinzani Bongo

Fahyma Bongo Fahyma

Sat, 20 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Fahyma au Fahyvanny; ni baby mama wa msanii Rayvanny ambaye anasema kuwa, ukizungumzia mastaa wanaojua kupendeza Bongo nzima, basi yeye hana mpinzani.

Fayma anasema kuwa, ukimtazama vizuri kwenye picha zake, unaweza kufikiri siyo Mtanzania kabisa maana unyamwezi ni mwingi. Fahyma anasema kuwa, anaogopesha, kiasi kwamba ukiwa mwanaume, huwezi kutamani kutoka naye kimapenzi maana anaonekana ni wa bei ghali mno.

Hivi karibuni, Fahyma alidai kuwa, uzuri wake umeongezeka maradufu hivyo mahari imeongezeka kwa mwanaume yeyote mwenye mpango wa kumchumbia na kumuoa.

Fahyvanny ambaye wengi walimjua kutokana na kuchumbiana na msanii Rayvanny au Vanny Boy kiasi cha kutumia jina la msanii huyo na kuunda lake anasema kwamba uzuri wake kwa siku za hivi karibuni umezidi kunoga na bei ya mahari haitabaki palepale ilipokuwa kwani nayo lazima itii na kuongezeka vilevile.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live