Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fahyma: Sasa najinenepea tu

Fahyma Bongo Fahyma

Sat, 29 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Fahyma; ni mwanamitindo na baby mama wa staa wa Bongo Fleva, Rayvanny au Chui ambaye kwa sasa anasema kuwa ana furaha kiasi kwamba anajinenepea tu kila siku baada ya kurudiana na jamaa huyo ambaye walitengana kwa takriban mwaka mmoja.

Walipotengana, Rayvanny alikwenda kupooza moyo wake kwa mrembo barobaro, Paula Kajala, kabla ya mambo kuharibika na kurejea kwa mama wa mtoto wake, Fahyma.

Fahyma anasema kuwa, anashangaa kwani amejikuta mwili wake ukiongezeka kwa kasi ya ajabu na kuwa kibongekibonge.

Siri hiyo imevujishwa na shoga’ke Fahyma ambaye ni Muna Love anayesema kunenepa kwa modo huyo kunatokana na furaha ya kurudiwa na Rayvanny au V Vany Boy.

Kumbukumbu zinaonesha kuwa, kipindi kile alichoachwa, Fahyma alikonda mno, lakini sasa nuru imerejea.

Si tu kumrudia, bali Rayvanny anatajwa kumfungulia Fahyma biashara ya kope bandia ambayo si haba inafanya vizuri na kumuingizia mkwanja mrefu kiasi cha kurushiana vijembe na Paula anayemiliki duka la nguo.

Kwa mujibu wa Fahyma, asilimia zaidi ya 70 ya biashara hiyo amewezeshwa na mpenzi wake ambaye kila mtu anajua ni Rayvanny na si mtu mwingine.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live