Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fahyma: Rayvvany I Miss You

Fahyma Rayvanny Fahyma na Rayvvany

Tue, 18 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

FAHYMA ni mwanamitindo wa kimataifa wa Tanzania, ni modo, fashenista, mjasiriamali, balozi wa brandi mbalimbali, sosholaiti, mwigizaji, dansa, video-vixen, mtangazaji na baby mama wa msanii Rayvanny ambaye amejaaliwa naye mtoto mmoja wa kiume aitwaye Jaydanny.

Fahyma ni mwanamama aliyepevuka akitumia nguvu nyingi kuhakikisha anaishi maisha yake ya kujitegemea bila kumtegemea mtu.

Fahyma ni miongoni mwa wanawake wachache wa Kitanzania wanaojua wanataka nini kwenye maisha hivyo kujituma hadi kujituma tena kufanya kazi ili kufikia malengo, tofauti na baadhi ya mastaa wengine wa kike ambao wamekuwa wakiishi kwa nguvu ya skendo za kudanga.

Inafahamika kwamba, Fahyma ni eksi wa Rayvanny ambaye alinyang’anywa tonge mdomoni na Paula Kajala. Hata hivyo, Fahyma amekuwa akionesha ishara za kwamba bado anampenda Rayvanny kwa kigezo cha kulea mtoto wao.

Katika hali hiyo, Rayvanny ameachia ngoma mpya ya I Miss You aliyomshirikisha Zuchu ambap ndani yake jamaa huyo anaelezea namna ambavyo amemmisi eksi wake, Fahyma akimuomba amsamehe na kusahau yaliyopita, yaliyosababisha watemane.

Katika ngoma hiyo, Rayvanny anasisitiza kuwa amemmisi mno Fahyma hivyo anamuomba arudi kwenye maisha yake kwani maisha yalikuwa bomba mno walipokuwa wawili.

Rayvanny anamuahidi Fahyma kwamba hatamuumiza tena akimtaka wayamalize na warudi kama zamani kwani ndiye aliyekuwa anamfanya ayafurahie maisha.

Saa chache tu baada ya ngoma hiyo kuanza kutrendi huko TikTok ndipo Fahyma akamjibu Rayvanny kupitia Insta Story yake kwa kumuambia; “I Miss You” akisindikiza na emoji za makopa akimaanisha naye amemmisi mno.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live