Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fahyma Paula Mwisho wa Ubishi

Fahyvanny, Rayvanny Na Paula Fahyma, Paula mwisho wa ubishi

Sat, 27 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

WAREMBO wawili maarufu Bongo wanaozungumzwa zaidi juu ya ni nani anayejua kuvaa kuliko mwingine, Fahyma na Paula Kajala; ubishi huo unakwenda kufikia mwisho ‘soon’.

Fahyma ambaye ni baby mama wa msanii Rayvanny aliyeporwa tonge kinywani na Paula; wawili hao wanawania tuzo kwenye Kipengele cha Female Stylish Personaliy of the Year 2021 kupitia Tuzo za Swahili Fashion Week zitakazofanyika Serena Hotel jijini Dar kati ya Desemba 3 hadi 5, 2021.

Pamoja na kwamba kuna wengine wakali kama Hamisa Mobeto na Jokate Mwegelo, lakini ushindani mkubwa unatajwa kuwa kwa Fahyma na Paula kutokana na kile kinachoendelea kati yao; kudaiwa ‘kushea’ mwanaume ambaye ni Rayvanny.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live