Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fahamui siri ya Celine Dion kukondeana

Celine Dion Fahamui siri ya Celine Dion kukondeana

Tue, 16 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwimbaji maarufu wa muziki Celine Dion aliolewa Desemba 17, 1994 na Rene Angelil ambaye pia alikuwa meneja wake, katika ndoa yao walijaliwa kupata watoto watatu ambao wote walipatikana kwa njia ya upandikizaji ijulikanao kama In Vitro Fertilization (IVF).

IVF ni utaratibu wa kutoa mayai kwenye ovari ya mwanamke na kukutanishwa na mbegu za kiume nje ya mwili ili kuunda kiini tete ambacho hukuzwa kwenye maabara kwa muda fulani na kuja kuwekwa kwenye mfuko wa uzazi wa mwanamke.

Kumpoteza mume wake, kaka yake, kukaza kwa misuli, upotevu wa sauti na kulea watoto mwenyewe vinatajwa kumpa sana msongo wa mawazo kiasi cha kuhatarisha afya yake, ingawa mwenyewe hapendi kuweka wazi hilo.

Dk Joachim Mabula kutokea Barrow Neurological anasema msongo wa mawazo una nafasi kubwa ya kudhoofisha hali ya mtu kiafya, lakini ni vigumu kusema ndio unapelekea kukaza kwa misuli.

“Msongo wa mawazo unaathiri afya kiujumla, ina maana furaha yake na uwezo wa mtu kujumuika na watu wengine, kwa hiyo itaathiri pia ratiba ya kula, lakini sio kwamba moja kwa moja inasababisha kukaza misuli,” anasema.

Mwaka 2019 Celine akizunguza na ABC News alisema: “Ni kweli mimi ni mwembamba kidogo, kila kitu kipo sawa, hakuna kitu kipya, ninafanya hivi kwa ajili yangu, nataka kujisikia mwenye nguvu na mwanamke mrembo zaidi,” alisema Celine. Mfahamu Celine Dion.

Huyu ni mwimbaji wa Pop, Rock, R&B, Gospel na Classical Music, alizaliwa Machi 30, 1968 huko Charlemagne, Quebec nchini Canada, akiwa mtoto wa mwisho katika famili ya watoto 14.

Celine akiwa na miaka 12 alikutana na Rene Angelil ambaye alivutiwa na kipaji chake na kuanza kumsimamia hadi kuachia albamu yake ya kwanza, ‘La voix du bon Dieu’ mwaka 1981. Alipofikisha miaka 19 wakachumbiana, kufikia mwaka 1994 wakati Celine akiwa na miaka 25 wakafunga ndoa.

Ametoa albamu tisa za Kirafansa na anashikilia rekodi ya msanii wa Kifaransa aliyeuza zaidi wakati wote, baada ya kujifunza Kiingereza, alijiunga na Epic Records nchini Marekani mwaka 1990, alitoa albamu yake ya kwanza ya lugha ya Kiingereza, ‘Unison’ iliyompa mafanikio makubwa hadi kushinda tuzo ya Grammy.

Nyimbo zake tangu wakati huo zimekuwa za Kiingereza na Kifaransa, ingawa pia ameimba Kihispania, Kiitaliano, Kijerumani, Kilatini, Kijapani na Kichina.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live