Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fahamu undani wa sakata la Diamond kupima DNA na mtoto wa Mobeto

Mobeto Diamond Mama D Fahamu undani wa sakata la Diamond kupima DNA na mtoto wa Mobeto

Thu, 18 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Oktoba 2020, mwanamama Hamisa Mobeto alithibitisha tetesi za mzazi mwenzake, Diamond Platnumz kuchukua vipimo vya DNA na mwanawe Dylan baada ya maneno kuzidi kusambaa juu ya mtoto kuwa ni wa msanii Jaguar wa Kenya.

Mjadala huo umerudi upya baada ya Hamisa kuondoa utambulisho wa Diamond kwenye jina la mtoto huyo baada ya kudaiwa kumtelekeza siku ya birthday yake, Agosti 8, mwaka huu.

Katika majibu yake ya Oktoba, 2020, ni kweli yeye na Diamond walifanya vipimo vya DNA hivyo ili kujihakikishia na majibu yalitoka asilimia 100% mtoto huyo ni wa Diamond.

Hamisa alisema; “Tulikwenda hospitalini na tukachukuliwa vipimo vinnevinne, wakasema tusubirie wiki mbili au tatu na majibu yakatoka mtoto kwa asilimia zote 100% ni wa Diamond…”

Hata hivyo, juu ya sakata hilo, mama mzazi wa Diamond, Mama Dangote amekuwa akitupiwa lawama kuwa ndiye chanzo cha mtoto wa Hamisa kutelekezwa na Diamond kwa sababu za ugomvi wao binafsi.

Baadhi ya watu wameendelea kumtetea mtoto huyo kuwa hana makosa hivyo kuendelea kufanya hivyo ni kumuumiza malaika wa Mungu asiyejua lolote.

Wanasema kuwa, ifike mahali Mama Dangote aachane na bifu na Hamisa amkutanishe mtoto huyo na watoto wengine wa Diamond la sivyo dhambi hiyo itamtafuna. Watu hao wanaohoji ni kosa gani mjukuu wake huyo alimtendea ambalo halisameheki?

Wanamtaka Diamond kuonesha msimamo kwa watoto wake kwa sababu wakati akiwatafuta alikuwa yeye na mwanamke husika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live