Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

SIL

Fahamu spishi 5 za binadamu zilizowahi kuishi ambazo huenda huzifahamu

Species Huma Fahamu spishi 5 za binadamu zilizowahi kuishi ambazo huenda huzifahamu

Thu, 10 Oct 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tumezowea sana wazo la kuwa sisi ndio watu pekee katika sayari kiasi kwamba ni vigumu kufikiria kwamba si muda mrefu sana katika historia ya mabadiliko yetu, aina mbali mbali za binadamu waliishi katika ardhi yetu.

Paleolithic au mazingira ya zama za mawe yalikuwa ya mabadiliko ya mara kwa mara. Watu walihama, walichangamana na wakati mwingine hata kuchanganyikana.

Kutokana na upatikanaji rahisi wa mbinu za kisasa za kiakiolojia, tunaweza ''kuona'' maisha ya wanadamu hawa kwa ufanisi zaidi, na kuufanya ulimwengu wa zama za mawe kuonekana kama mchoro unaoishi kuliko kipande cha masalia kilichowekwa katika makumbusho ya vitu vya kale.

Lakini ni aina ngapi tofauti za binadamu ambao waliwahi kuishi duniani? Hili ni swali kubwa, na wanaakiolojia bado hawajaweza kukubaliana.

Sehemu kubwa ya mjadala ni kwamba kuna spishi chache ambazo wanaakiolojia wanaweza kuzifanyia kazi.

Watafiti wameweza kufukua masalia ya miili ya watu wa kale ipatayo 6,000 na ni michache kati yake iliyoweza kutoa ushahidi wa jeni.

Miongoni mwa mambo mengine, waliyojaribu kubaini ni kujaribu kuelewa ni masalia gani ya kale yanawakilisha spishi gani mpya, wakati mwingine kutoka kwenye fuvu moja au mfupa wa kidole cha mkono.

Hizi ni aina za spishi ambazo zimechangia katika historia ya mabadiliko ya binadamu, ambazo huenda usizifahamu, na ambazo zinaonesha ni kwa jinsi gani binadamu wa kale walivyoishi katika maeneo mbali mbal.

1. Homo Rudolfensis

Homo rudolfensis ni mfano mzuri wa hatari za kuwaelezea spishi kwa kuzingatia ushahidi wa ukomo wa masalia ya miili ya kale.

Jina lake lilizingatia binadamu mmoja, fuvu, pia akifahamika kama KNM-ER 1470, ambaye aliishi takriban miaka milioni 1.9 iliyopita na alitokea eneo la Koobi Fora, ambalo kwa sasa ni Kenya.

Awali, fuvu lilisemekana ni la spishi wanaoitwa Homo habilis, ambaye ndiye aliyekuwa kizazi cha zamani kabisa cha binadamu. Hatahivyo, kulikuwa na baadhi ya matatizo na hili : Kwanza fuvu ilikuwa kubwa sana.

Masalia mengine ya Homo habilis yalikuwa na ubongo wa kilomita za ujazo zipatazo 500; Homo rudolfensis walikuwa na mafuvu ambayo yangeweza kuhifadhi ubongo wenye ukubwa wa sentimita 700 za ujazo.

Masalia H. rudolfensis pia yalikuwa na meno mapana na mfupa mdogo sana wa juu ya macho .



Wataalamu wa mienendo na tabia za kihistoria za binadamu (wanaanthropolojia) hatimaye waliafikiana kuwa huenda hizo zilikuwa ni aina mbali mbali za spishi moja-na hata wakazingatia uwezekano wa kuwepo kwa tofauti kati ya wakike na wa kiume-kama sababu ya tofauti hizi za kimaumbile.

Hii ndio maana KNM-ER 1470 ilipokea spishi ya pili tofauti katika mwaka 1986.

2. Homo antecessor

Pango kubwa la Dolina ama The Gran Dolina Cave lililopo eneo la Atapuerca, nchini Uhispania, ni eneo kubwa la kiakiolojia, likiwa na ukubwa wa mita 20 na limekuwa na historia ya zaidi ya miaka nusu milioni.

Eneo hili limedumu kwa karibu miaka 780,000 na linajumuisha masailia ya kikundi cha spishi cha binadamu aina ya hominids ambao walipewa jina la Homo antecessor katika mwaka 1997.

Spishi hawa mara kwa mara huelezewa kama waliokuwa na mchanganyiko wa maumbile ya kisasa na "ya kizamani" : Baadhi ya viungo vyao na tabia vinafanana na vile vya spishi za Neanderthals na Denisovans, huku wengine wakifanana na Homo sapiens.

Utafiti wa hivi karibuni kuhusu protini za kale zilizochukuliwa kutoka kwenye meno ya mojawapo ya mabaki ya spishi aina ya Atapuerca zimeonyesha kuwa H. antecessor ni "dada" wa karibu mwenye uhusiano na mwanadamu wa sasa pamoja na, Neanderthals, na Denisovans.

Binadamu hawa kwa pamoja wana mababu wanaofanana wa karibu

3. Homo floresiensis

Masalia pekee ya kale yanayofahamika ya Homo floresiensis yalipatikana katika pango la Liang Bua lililopo katika kisiwa cha Flores, nchini Indonesia .

Wanaakiolojia pia wanawaelezea spishi hawa kama "hobbits", ama binadamu wanaotoka kwenye jamii moja kwasababu ya urefu wao unaofanana: wote walikuwa na urefu wa zaidi kidogo ya sentimita 90.

Masalia ya kwanza ya H. floresiensis yaligundulika mwaka 200.3

Binadamu hawa ndugu walikuwa na ubongo mdogo (wenye ukubwa wa takriban sentimita 400 za ujazo), lakini waliwinda na zana zao zilikuwa zinafanana sana na zile zilizotengenezwa na Homo erectus, spishi ambazo zilikuwa na ubongo mkubwa.

4. Homo luzonensis

Mabaki mengine ya binadamu wa kale yaligundulika hivi karibuni luzonensis Homo, ambao waliishi kwenye kisiwa cha Luzon, nchini Ufilipino, miaka takriban kati ya 50,000-60,000 iliyopita.

Fuvu na meno ya Homo luzonensis

Spishi hii inawakilishwa na mifupa 13 pekee: meno, vidole vya mikono na vya miguu, pamoja na mfupa wa paja. Masalia haya ni kutoka kwa watu watatu.

Katika mwaka 2019, wanaanthropolojia walibaini kuwa mifupa ina utofauti wa mkubwa wa kutosha na ile ya spishi wengine kama H. erectus na H. floresiensis kwa kiwango cha kutosha kuweza kuwaweka katika aina nyingine ya spishi.

Kidole na mfupa wa mguu vya H. luzonensis vinashangaza.

Vimejipinda kidogo, tabia inayofanana na ile ya spishi wanaoishi katika miti na hivyo kuibua dhana kwamba H. luzonensis huenda ilikuwa ni sehemu ya mtindo wao wa maisha.

5. Homo Longi (dragon man)

Spishi wanaopendekezwa kuwa ni wa hivi karibuni zaidi wa binadamu wa kale wanatoka katika Uchina, ambako fuvu lao kubwa zaidi lilipewa jina la "Dragon Man" mwezi Juni.

Fuvu hilo kwa mara ya kwanza lilipatikana katika miaka ya 1930, lakini ni hivi tu karibuni liliweza kupatikana kwa ajili ya kutathminiwa na wanasayansi.

Inasemekana iliishi miaka karibu 146,000, na wale wanaotathmini wanalielezea kama " dada aliyepotea kwa muda mrefu" H. sapiens (wa binadamu).

Hatahivyo, ukubwa wa ubongo unaweza kulinganishwa na ule wa binadamu wa sasa. Uvumbuzi huu mpya ni ukumbusho mwingine wa kazi ngumu ya kutafuta spishi wengine wapya wa binadamu.

Ukweli ni kwamba "Dragon Man" huenda akawa Denisovan, ila kwa sasa hakuna ushahidi wa jeni wa kusaidia kubaini hilo.

Kila mtu mmoja anapogundulika kuwa katika matawi ya familia ya binadamu, anatukumbusha kuwa maisha ya kale ya binadamu yanakanganya na bado kuna mengi ya kujifunza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live