Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Fahamu simulizi ya kusisimua ya maisha ya Steven Hawking

Steven Hawking Fahamu simulizi ya kusisimua ya maisha ya Steven Hawking

Mon, 18 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Steven Hawking akiwa kijana mdogo wa umri wa miaka 21 alipata ugonjwa wa Amyotrophic Lateral Sclerosis (ALS)), Ugonjwa ambao ulimfanya mwili kupooza na matokeo yale akawa hawezi kutembea tena na baadae akapata tatizo la kushindwa kuongea. Matatizo haya aliyapata akiwa ana ndoto kubwa ya kuwa mwanasayansi.

Kutokana na changamoto hizo za maradhi alizozipata Steven Hawking ilibidi awe anatembea kwa kutumia kiti chenye magurudumu na kuongea kwa kutumia program maalum ya kompyuta ambayo ilitengenezwa kwa ajili ya kumsaidia katika shughuli zake za kila siku.

Steven Hawking licha ya kutembea kwa kutumia kiti cha magurudumu na kuongea kwa kutumia programu wezeshi ya kompyuta kwa zaidi ya miaka hamisi, hakuwahi kuvunjika moyo aliamini ndoto zake zilikiwa kubwa kuliko matatizo aliyonayo.

Steven Hawking aliendelea kusoma kwa bidii na kufanya tafiti mbalimbali za kisanyansi na akafanikiwa kufika daraja la kuwa professa na kuandika kitabu maarufu cha kisayansi kinachoitwa Brief history of Time.

Steven Hawking akiwa kwenye kiti cha magurudumu alipewa tuzo lukuki jina lake likawa kubwa akafanya mikutano mikubwa ya kisayansi na ilipofika march 14,2018 pale kwenye maeneo ya Cambridge nchini uingereza alilala usingizi wa milele akiwa hana deni lolote lile kwenye ndoto zake.

Kabla Profesa Steven Hawking hajaondoka juu ya mgongo wa ardhi alisisitiza mambo haya.

1.Tuishi kwa matumaini

2.Ulemavu sio mwili ni kushindwa kuifanya akili yako kuuzunguka ulimwengu.

3.Hakuna mipaka kwenye jambo lolote lile.

4.Tupende kutafuta njia za kutatua matatizo na kuacha lawama.

NB.

Wewe ni mzima wa afya haupo kwenye kiti cha magurudumu na bado unalaumu watu na matukio na mbaya zaidi unataka ndoto zako watimize watu wengine.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live