Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

SIL

Fahamu sifa tano za 'wife material'

Happy Looking Couple In Bed Fahamu sifa tano za 'wife material'

Tue, 26 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wiki hii nitazungumzia sifa tano za mwanamke ambaye anastahili kuwa mke au kwa kizungu tunasema ‘wife material’. Nafanya hivi ikiwa ni msaada kwa wale ambao wamefikia hatua ya kuingia kwenye ndoa lakini bado wanashindwa kutambua yupi ni sahihi na yupi si sahihi kuitwa mke.

Tufahamu kwamba si kila mwanamke unayekutana naye na ukaonesha kumpenda anafaa kuwa mkeo. Wengine wana upungufu ambao bila kuubaini na ukaingia kichwakichwa, utakuja kujuta siku moja.

Ndiyo maana nikaona leo kupitia hapa nikupe sifa 5 za msichana ambaye anafaa kuwa mkeo. Mengine utajiongeza mwenyewe.

AKUPENDE KWA MAANA HALISI YA KUKUPENDA

Unapoingia kwenye maisha ya ndoa, unatarajia kupata mapenzi ya kweli kutoka kwa mwenza wako. Wapo baadhi ya wanawake ambao wanaonesha wazi kutokuwa na mapenzi ya kweli bali wanakuwa na mapenzi ya kuzuga.

Wanachotaka wao ni aidha kupata umaarufu tu kwamba yuko na mtu fulani ama kuweza kupata pesa alizonazo mwanaume lakini sio kwamba ana mapenzi ya dhati kutoka moyoni mwake.

Kwa nini ni vizuri kumpata mwanamke mwenye mapenzi ya dhati kutoka moyoni na si kwamba akupende kutokana na mali au fedha zako na muonekano wako? Hii inatokana na ukweli kwamba maisha siku zote yanabadilika, kuna kupanda na kushuka.

Sio kwamba kila siku utakuwa na maisha mazuri na kama itatokea hivyo basi ushukuru Mungu. Hivyo basi mwanamke wa kuoa lazima afahamu hivyo na awe tayari kuonesha mapenzi yake ya dhati wakati wote wa maisha yenu.

HILI LA TABIA NDO’ KILA KITU

Linapokuja suala na kuoa, tabia inakuwa kitu cha awali sana kuangaliwa. Hii ni kwa sababu, wapo wasichana wazuri wenye mvuto wa aina yake na maumbile mazuri, lakini wanakosa sifa ya kuitwa mke kutokana na tabia zao chafu.

Hakuna mwanaume anayeweza kudiriki kumpa nafasi msichana kuwa mke wake wakati ana tabia chafu. Endapo utaangalia uzuri wa sura kisha ukafanya maamuzi ya kuoa, utakuwa unajichimbia kaburi.

AOTE MAFANIKIO

Hivi karibuni kume-kuwepo na mabadiliko ya aina yake kwa wanaume, wengi sasa hivi hawapendi kabisa kuoa mwanamke ambaye hana kazi ‘golikipa’.

Kama atakuwa hana kazi basi awe na uchu wa mafanikio kwa kujituma kufanya kazi mbalimbali za kimaendeleo kama vile kilimo kwa wale walio vijijini na biashara ndogondogo kwa wale ambao wako mijini na hata vijijini.

Ile dhana ya kuoa mwanamke kwa ajili ya kukustarehesha tu imepitwa na wakati. Hizi ni zama za kutafuta mtu wa kushirikiana naye kwenye kusaka mafanikio.

UVUMILIVU

Wapo wanawake ambao sio wavumilivu kabisa katika maisha. Tunajua kwamba maisha siku zote hayatabiriki, yanaweza kutokea matatizo ya kiafya ama kifedha. Huu ndio wakati wa kuona uvumilivu wa mtu.

Kama mwanamke anatarajia kwamba siku zote ni za raha tu na pindi matatizo yanapotokea anachukua uamuzi wa kumtoroka mwanaume, huyo siyo mwanamke wa kuoa.

Wangapi leo hii huwatoroka waume zao pindi wanapoumwa, kufilisika ama kupatwa na tatizo lolote ambalo kwa namna moja ama nyingine linaweza kuwafanya maisha yao kutingishika?

Uvumilivu kwa mwanamke utakuwepo kama tu atakuwa na mapenzi ya dhati kama nilivyozungumza hapo awali. Mwanamke mwenye mapenzi ya dhati ni lazima atakuwa mvumilivu na atakuwa tayari kuishi katika maisha ya aina yoyote, yawe ya raha ama ya starehe. Hawa ndio wale ambao wanaume wengi wengependa kuwa nao maishani mwao.

HANA MAKUZI

Kuna wanawake wengine wanakuwa na tabia za ajabu sana kiasi kwamba yaweza kuwa kero kwa wanaume. Wapo wanawake ambao wanapenda makuu bila kujali hali halisi ilivyo. Wa kumuoa hatakiwi kuwa hivyo.

Anatakiwa kuwa tayari kula dagaa pale inapobidi na kama uwezo wa kula nyama upo basi atakula. Awe tayari kutembea kwa miguu pale usafiri wa maana utakapokosekana, awe tayari kuvaa nguo za kawaida, awe tayari kutumia simu ya tochi.

Kwa kifupi mwanamke ambaye ni ‘wife material’ anatakiwa kuwa tayari kuishi maisha ya aina zote. Tukutane tena wiki ijayo kwa mada nyingine.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live