Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Fahamu pishi la kuchemsha mayai kwa kutumia haja ndogo

TRANT377LXROACC7MQRLHIOSA4 Fahamu pishi la kuchemsha mayai kwa kutumia haja ndogo

Wed, 6 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Duniani kuna tamaduni nyingi, zinazohusisha jamii mbalimbali, wakati huohuo katika jamii husika huziona ni sawa lakini zikienda kwenye jamii yingine watu huziona kama kituko.

Ukizungumzia China kwenye upande wa vyakula utakutana na aina nyingi zipatikanazo nchini humo, ambavyo watu kutoka mataifa mengine hushindwa kuvila na kuviona vya ajabu.

Imezoeleka kuwa watu hutumia maji kuchemsha mayai lakini leo fahamu kuwa nchini China kuna tamaduni ya kuchemsha mayai kwa kutumia haja ndogo ya wavulana walio chini ya miaka 10, ambao bado hawajawahi kushiriki vitendo vya ngono. Mayai hayo huchemshwa na haja ndogo kwa sababu maalumu na hupendwa na watu wengi nchini humo.

Wafanyabiashara wa mayai hayo hutumia mbinu mbalimbali kupata haja ndogo ya kuchemshia kama vile kupeleka madumu ama ndoo kwenye shule za msingi ambazo wanapatikana watoto wenye umri chini ya miaka kumi na kisha hutumia haja hiyo kuchemsha mayai hayo na kisha kuyauza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live