Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fahamu mambo 10 toka kwa Dudu Baya

Dudubaya Dudu Baya

Mon, 15 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

1. Baada ya kumpiga Mr. Nice kulipeleka yeye kufunguliwa kesi mahakamani, hivyo alikuwa haruhusi kusafiri nje ya nchini.

Kutokana na hilo kulipelekea yeye kukosa show tatu nchini Uingereza, miongoni mwa wasanii walioenda kwenye show hizo ni Ray C, Mandojo na Domo Kaya.

2. Producer kutokea MJ Records, Master Jay ndiye producer aliyetengeneza nyimbo nyingi zaidi za Dudu Baya ikiwemo Mwanangu Huna Nidhamu iliyotoka mwaka 2000.

3. Dudu Baya kupitia lebo yake Dar Skendo alimuwezesha msanii Besta kuanza kusikia zaidi Tanzania baada ya kumaliza masomo yake nchini Uganda.

Muimbaji huyo wakati anamtafuta Dudu Baya alikuwa ametoa wimbo uitwao Baby Boy baada ya kutoa ngoma na Dully Sykes. Besta kwa sasa ni mke wa msanii Marlow na pia ni mama wa watoto kadhaa.

4. TID alitaka kukataa kushiriki kwenye wimbo wa Dudu Baya uitwao Inuka lakini baada ya kumsikilizisha verse ya wimbo huo ndipo akakubali.

5. Dudu Baya anamtaja Tupac kama msanii aliyemvutia zaidi hadi kuingia kwenye muziki, mwingine ni rapper DMX, wote hawa ni kutokea nchini Marekani.

6. Dudu Baya amewahi kutangaza mara mbili kuacha pombe, October 2011 alifanya hivyo na December 2018. Hivyo alichotangaza awali utekelezaji wake haukufanikiwa.

7. Licha ya Dudu Baya kufanya vizuri na nyimbo kama Mwanangu Huna Nidhamu, Nakupenda Tu, Tentemente (mpenzi), ila wimbo pekee anaoupenda zaidi kutoka kwake ni ule uitwao Nimeondoka.

8. Dudu Baya ndiye aliyemtambulisha Sister P kwenye muziki baada ya kumshirikisha kwenye wimbo wake uitwao Kunguru Hafugiki wimbo ambao ulibeba albamu yake ya kwanza inayokwenda kwa jina la Kitu na Box.

Baada ya hapo ndipo Sisiter akaenda kurekodi wimbo wake wa kwanza Bongo Records kwa producer P Funk Majani, wimbo huo unaitwa Nakuja.

9. Dudu Baya aliwahi kumkataza Chege kutumia jina la Konki Master kitu ambacho kilitafsiriwa kama wana bifu lakini wawili hawa mwaka 2013 walitoa wimbo mmoja uitwao Wakaka.

10. wimbo wa Dudu Baya uitwao Mpenzi (Tentemente).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live