Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Fahamu maiti iliyolindwa zaidi duniani

Vladimir Lenin Vladimir Lenin.

Mon, 4 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Vladimir Ilyich Ulyanov, anafahamika zaidi kama Vladimir Lenin alifariki Januari 1924, viongozi wengi wa Sovieti walipinga wazo la kuhifadhi mwili wake zaidi ya kipindi cha muda cha maonyesho kwa umma.

Lenin alihudumu kama mkuu wa Urusi ya Soviet kuanzia 1917 hadi 1922 na kama mkuu wa Muungano wa Sovieti kuanzia hadi kifo chake, uwezekano mkubwa wa kilo chake kutokana na mshtuko mkubwa wa kiharusi, mnamo 1924. Alikuwa na miezi michache tu kabla ya kutimiza miaka 54.

Kifo chake kiliwapa viongozi muda wa kufikiria upya wazo la kukihifadhi mwili wa kiongozi huyo kwa muda mrefu zaidi. Ili kuepuka uhusiano wowote wa mabaki ya Lenin na masalio ya kidini, walitangaza ukweli kwamba sayansi na watafiti wa Sovieti walikuwa na jukumu la kuihifadhi na kuitunza.

Takriban miaka zaidi ya 100 baada ya kifo chake na zaidi ya miaka 25 baada ya Muungano wa Kisovieti kuvunjwa, mwili wa kiongozi wa Kisovieti Vladimir Lenin bado uliwekwa wazi kwa umma Red Square huko Moscow mbele ya Ikulu ya Kremlin.

Hapo awali, mwili wa Lenin ulipaswa kuonyeshwa hadharani kwa muda mfupi na kisha kuzikwa kulingana na matakwa ya Lenin. Hata hivyo, viongozi wa Umoja wa Kisovyeti waliamua kuweka mwili uhifadhiwe ili uwe historia kwa vizazi

Kuhifadhi mwili kunaashiria zaidi ya miaka 90 ya mafanikio ya kisayansi. Kazi hiyo imefanywa na timu ya wanasayansi kutoka Taasisi ya Mimea ya Dawa huko Moscow. Timu hii pia imefanyia kazi miili ya viongozi wengine kama vile Ho Chi Minh wa Vietnam, Agostinho Neto wa Angola na Kim Il-sung wa Korea Kaskazini.

misururu mirefu ya watu ambao bado walitaka kumuaga kiongozi wao; zaidi ya watu 500,000 takati huo walikuwa tayari wamepanga foleni kutoa heshima zao. Baada ya majadiliano mengi, Chama kwa pamoja kiliamua kwamba kaburi lenye mwili wa Lenin liwe mahali pa kuhiji ulimwengu kwa tabaka la wafanyakazi na urusi.

Pengine ungeshtuka kujua kwamba si lazima hata uwe hai na uhesabiwe kuwa wa thamani na unaostahili kulindwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live