Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fahamu machache kuhusu Nikki Mbishi

Niki Mbishi Fahamu machache kuhusu Nikki Mbishi

Mon, 11 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ngoma yake, Play Boy kutoka kwenye albamu yake ya kwanza, Sauti ya Jogoo (2011) chini ya M Lab (Music Laboratory), ililitangaza vyema jina la Nikki Mbishi.

Wakati anaanza muziki alikuwa akijiita 'Nikki Jay' akijifananisha na 'Nigga Jay' ndipo akaja kubadil jina hilo baadaye na kuwa NIKKI MBISHI.

Katika kipindi cha miaka 15 iliyopita, MBISHI ndiye msanii peke Bongo aliyetoa albamu nying zaidi. Alitoa albamu tano ambazo ni Saut ya Jogoo, Malcom XI, Ufunuo wa Unju Bin Unuq, Sam Magoli na Welcome to Gamboshi, huku akitoa Mixtap moja, K.I.G.U (Kisirani Ghubu cha Unju).

katika shindano la Kilimanjaro Emcee Shujaa (2008) MBISHI alikuwa mshindi wa pili, Lusajo wa kwanza na Godzilla wa tatu, hiyo ni baada ya NIKKI na ZILLA kushindwa kufua dafu kwenye shindano la Sprite Emcee Africa chini ya Channel O.

Utakumbuka Nikki na Zilla wameshirikiana kwenye ngoma kama Kila Siku, Kill Yo Self, SISI na nyingine.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live