Je, Unafahamu nini kuhusu Miruko Mzimu (Ghost Flight) au ndege tupu? Mamia ya ndege huruka tupu huko Ulaya kila mwezi. Hizi zinaitwa ndege tupu au "Ghost flights"
Takwimu zinaonyesha kuwa kumekuwa na 'safari nyingi kama hizi za ndege' huko Amerika Kusini au Caribbean katika miaka michache iliyopita.
Pamoja na ujio wa janga la Corona na kuongezeka kwa vikwazo vya usafiri, tatizo hili limezidi katika kanda hiyo.
Viwanja vingi vya ndege vinapaswa kuweka asilimia 80% ya safari za ndege zilizopangwa ili kuendelea kudumisha nafasi zao za kupaa na kutua na asilimia 20% za kughairiwa safari za ndege.
Ikiwa safari za ndege hazitimizi matakwa ya asilimia hizi, mashirika ya ndege yatalazimika kuruka kwa kutumia ndege tupu ili kudhibiti nafasi kwenye viwanja vya ndege bila kughairi safari zilizopangwa.
Vinginevyo, wanaweza kuhatarisha kuporwa 'nafasi za muda bora zaidi za kibiashara' kwenye viwanja hivyo vya ndege mwaka unaofuata.
Ndege zinahitaji kuruka na kutua muda ambao hautakuwa wa mateso kwa abiria na upatikanaki wa 'connection' ya abiria kutoka sehemu mbalimbali.
"Uitumie au uiache" Tume ya Ulaya na Shirikisho la Usafiri wa Anga (FAA) ya Marekani hutumia sheria ya "kutumia nafasi au iache'' ili kudhibiti kasi ya safari zote za ndege kwenye viwanja vya ndege vyenye shughuli nyingi zaidi.
Baraza la Kimataifa la Viwanja vya Ndege (ACI) linafafanua kama "Ndege tupu ni safari za ndege zinazoendeshwa kwa hiari na mashirika ya ndege ili kuhifadhi haki zao za maeneo yanayopangwa."