Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fahamu kuhusu Mavokali kusainiwa na Rayvanny

Mavokali Rayvanny Fahamu kuhusu Mavokali kusainiwa na Rayvanny

Mon, 9 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mafanikio ya Remix ya wimbo wa Commando wa @mavokali_ ambao humo ndani ameshirikishwa @rayvanny yamekuja na story kibao ikiwemo hii ya kumuhusisha @mavokali_ kuwepo kwenye mazungumzo ya kutaka kusainiwa na Record Label ya @nextlevelmusic_tz inayomilikiwa na Msanii @rayvanny.

Kwenye #CloudsFMTop20 leo @mavokali_ amekanusha kuhusu taarifa hizo na kueleza kuwa hajawahi kukaa na @rayvanny kulizungumzia hilo japo kuwa endapo itatokea haitazami kama ni biashara mbaya na atakuwa na utayari wa kukaa mezani kuzungumza kibiashara zaidi.

Story hizi zimezuka baada ya ukaribu wa Mavokali na Rayvanny siku za hivi karibuni ikiwa Mavokali anauelezea ukaribu huo unasababishwa na kazi nyingi ambazo wamekuwa wakifanya pamoja ukiachilia mbali Commando Remix ambayo tayari imekwisha achiwa.

Commando ya Mavokali imesimama nafasi ya 14 kwenye chati za #CloudsFMTop20 wiki hii.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live