Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fahamu kuhusu Mavokali kusainiwa WCB

Mavokaliiii Fahamu kuhusu Mavokali kusainiwa WCB

Thu, 2 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kama ulikuwa unadhani msanii mpya aliyesainishwa hivi karibuni na label ya WCB kuwa ni Mavokali hilo toa akilini mwako, Fella amekanusha sio msanii huyo waliyemsainisha.

Mkubwa Fella ambaye pia ni mmoja wa mameneja wa WCB amesema; "Kwanza sio yeye, halafu msanii (aliyesainishwa) anatoka Temeke ila simtaji, itakapofika wakati Nasib (Diamond) mwenyewe atamtaja," ameeleza Fella akiiambia Dizzim Online kwenye mahojiano yake mapya.

Itakumbukwa, hitmaker wa "Mapopo" msanii Mavokali aliingia kwenye headlines mnamo Februari 2, baada ya mchana wa siku hiyo, Boss wa lebo ya WCB, msanii Diamond Platnumz kuweka wazi ameingia mkataba na msanii mpya ambapo ali-share sehemu fupi ya picha katika mkataba huo na kuambatanisha ujumbe huu, "02/02/2023 Another Blessing day for the blessing kid".

Aidha, Diamond hakuweka wazi juu ya jina wala jinsia ya msanii huyo mpya na hata kuhusu lini atatangazwa rasmi, sasa saa chache baadae (siku hiyo hiyo) Mavokali kupitia insta story yake akaandika "02/02/2023 Deal Done" akiwa na maana tarehe 2 mwezi wa pili kuna dili amelikamilisha.

Hivyo, mashabiki na wadau mbalimbali wakawa wanauhusisha ujumbe huo wa Mavokali na taarifa mpya ya Diamond kuwa ndio ingizo jipya katika lebo hiyo ambayo hadi sasa ina jumla ya wasanii watano pekee.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live