Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fahamu Sababu ya Harmonize Kukimbiwa na Machawa

Harmonize Hbaba Harmonize na H Baba

Sun, 13 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kambi ya Mjeshi wa Konde Gang, Rajab Abdul almaarufu Harmonize inazidi kukimbiwa na machawa wake baada ya mkongwe wa Bongo Fleva, Hamis Baba au H Baba kumkimbia mapema wiki hii.

H Baba anaungana na orodha ndefu ya machawa waliomkimbia Harmonize kuanzia Mwijaku, Masha Love, Dokta Kumbuka, Aristote na wengineo.

Kabla ya kuchukua uamuzi huo, H Baba na Mwijaku waliapa kwamba kamwe hawawezi kumsaliti Harmonize kwa kuwa ndiye msanii namba moja nchini Tanzania.

Hata hivyo, imebainika kwamba, mara baada ya kuondoka kwa Harmonize, wote wamekimbilia kwa Diamond Platnumz au Wasafi kwa jumla.

Kuna sababu mbalimbali zinazotajwa kusababisha Harmonize au Harmo kukimbiwa na machawa hao ikiwemo ishu ya jamaa huyo kutomwaga pesa kama afanyavyo Diamond.

“Wanachofuata kwa Diamond ni pesa; muone Juma Lokole au Issa Azama, wanaendesha magari waliyopewa na Diamond. Wewe ulisikia lini Harmonize amepa chawa wake gari?

“Machawa wote wanamshangilia na kumpa mtu kwa sababu wanajua wanachokipata, yule Harmonize aana mkono mfupi na wenyewe wanasema mkono mtupu haulambwi,” anasema mmoja wa machawa hao.

Akizungumza na Gazeti la IJUMAA, Juma Lokole anasema kwa kuwa chawa wa msanii huyo, amepata ajira ya utangazaji wa Wasafi FM; kituo cha redio kinachomilikiwa na Diamond.

“Kwa sababu ukiwa chawa wa mtu maana yake unakuwa karibu naye, kwa hiyo ukiwa karibu na mtu mzito kama Diamond anakupa michongo ili akuunge mkono na kukutia nguvu. Anaangalia unaweza kufanya nini anakusapoti huko,” anasema Juma Lokole na kuongeza;

“Ukiwa chawa wa mtu mwenye pesa ya kununulia bia tu hakuna faida hapo. Kuwa chawa wa mtu ambaye anaweza kukupa mchongo mmoja tu ukabadilisha maisha yako.”

Naye Aristote ambaye ni chawa wa Diamond, Irene Uwoya na Fred Vunjabei anasema yeye ni chawa mwenye akili na mara nyingi hapendi kupewa pesa kupitia kuwa chawa; na hapa anafafanua namna anavyofaidika.

“Bosi kama Diamond akinipa pesa sikatai, lakini mimi siyo chawa wa kuombaomba pesa kwa sababu mimi siyo mlemavu, nina mikono yangu na naweza kufanya kazi.

“Faida kubwa ninayoipata kuwa chawa wa Diamond ni umaarufu ambao unafanya inakuwa rahisi zaidi kufanya biashara zangu za saluni na nyinginezo,” anasema.

Kwa mujibu wa machawa hao, hicho ndicho kinachofanya wamkimbie Harmonize na kwenda kwa Diamond ambako kuna faida kedekede.

Chawa ni mtu anayejipendekeza kwa mtu mwenye pesa au maarufu ili anunuliwe vitu vidogovidogo au naye apate umaarufu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live