Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fahamu Cheche ndiye aliyeingiza Kiswahili kwenye filamu maarufu ya Kirikou

Juma Rajabu Rashid Cheche Juma Rajabu Rashid na Cheche

Wed, 19 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Juma Rajabu Rashid maarufu kama Cheche mtungi ndiye aliyeingiza sauti ya #Kirikou kwa Lugha ya Kiswahili kwenye katuni hiyo pendwa barani Africa?

Cheche mtungi ni muigizaji na muongozaji cinema ameigiza filamu na tamthilia kadhaa ikiwemo ile iliyompa umaarufu ya Siri ya mtungi ikampa aka hiyo anayoitumia mpaka leo. Ingawaje wengi wetu tulimfahamu kupitia video ya wimbo wa #zoba ya Banana Zorro.

Pia anafanya kazi ya kuingiza sauti kwa lugha ya Kiswahili kwenye tamthilia mbalimbali za kigeni hasa hizi za Azam TV. Ikiwemo hiyo filamu ya kirikou ambayo origin yake ni lugha ya kifaransa.

Kweli jamaa ni fundi maana kwa tunaomjua jamaa ana sauti moja ya base flani hivi sasa linganisha na kile kisauti cha kirikou ambayo nina uhakika wote humu mshaiona filamu hiyo ambayo ni katuni inayowabamba mpaka watu wazima.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live