Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

FOA ya Diamond album bora ya mwaka AEAUSA

Screenshot 2023 01 01 185502.png FOA ya Diamond album bora ya mwaka AEAUSA

Mon, 2 Jan 2023 Chanzo: dar24.com

Mwaka 2022 umemalizika vyema na hatimaye mwaka mpya 2023 umeingia ukiambata na taarifa njema kwa nyota wa muziki wa bongo fleva Diamond Platnumz, ambaye kupitia extended playlist yake “First Of All (FOA) amefanikiwa kushinda tuzo ya album bora kwa mwaka 2022 kwenye tuzo za kimataifa za African Entertainment Awards (AEAUSA).

Tuzo hizo zimetolewa usiku wa kuamkia Januari 1, 2023 huko nchini Marekani.

Tuzo za AEAUSA kwa mwaka 2022, ni tuzo za nane kutolewa tangu kuanzishwa kwake ambapo ‘FOA’ ilifanikiwa kuchumpa kwenye kinyang’anyiro cha album bora za mwaka ikiwa katika ushindani mkali na album nyingine kama ‘Catch me if you can’ ya Adekunle Gold, ‘The Guy’ ya Mi Abaga, ‘Rave & Roses’ ya Rema pamoja na ‘Affection’ ya Magasco Bboy.

Taarifa za ushindi wa tuzo hiyo zimemfikia Diamond akiwa katika onyesho lake la funga mwaka (Cheers 2023) liliyofanyika usiku wa Desemba 31, 2022, Ramada hotel jijini Dar es salam.

First Of All EP, iliachiwa rasmi Machi 12, 2022 ikiwa na jumla ya nyimbo kumi, ambazo ndani yake ni takribani nyimbo nne pekee ndio alizoshirikiana na wasanii wengine akiwamo Adekunle Gold kutoka Nigeria, Mbosso, Zuchu pamoja na Jaywillz.

Chanzo: dar24.com