Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

SIL

FAHAMU: Ethiopia, Saudi Arabia ni nchi zisizotumia Red Carpet

Ethiopia Red Carpet (600 X 344) FAHAMU: Ethiopia, Saudi Arabia ni nchi zisizotumia Red Carpet

Tue, 29 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nchi nyingi zimekuwa na sifa mbalimbalia ambazo hutumika kama kielelezo chake, ukitaka kufahamu historia ya Ethiopia lazima ugusiwe kutotawaliwa kwake, na kuhusu Saudi Arabia lazima uelezwe kuhusu maua yenye rangi ya zambarau yaotayo jangwani.

Kuachana na kutotawaliwa kwa Ethiopia na maua yaliyopo Saudi Arabia, pia kumekuwa na sifa nyingine ya kipekee katika nchi hizo, za kutotumia zulia jekundu (red carpet), badala yake Ethiopia hutumia zulia la rangi ya kijani na maua ya njano, Saudi Arabia hutumia la zambarau.

Mazulia hayo nyenye rangi hizo hutumika katika matukio maalumu ya kitaifa, yakiwa na maana kubwa, Saudi Arabia hutumia rangi hiyo kuwakilisha maua ya asili yaliyopo jangwa la Saudi Arabia.

Ethiopia ni tofauti, huamini matumizi ya zulia la kijani ni sehemu ya sera ya maendeleo endelevu, matumizi ya teknolojia ya kisasa, kukuza historia, utamaduni, maadili na urithi wa Ethiopia. Zulia hilo hutengenezwa na kampuni ya Ethiopia, ‘Aklill Company’, wanaliita Adey Abeba Carpet.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live